Kikosi cha simba chawasili salama Dodoma,

October 3, 2020

 

KIKOSI cha Simba leo kimewasili salama mkoani Dodoma baada ya kuanza safari leo mapema kwa basi kikitokea Morogoro ambapo kiliweka kambi jana, Oktoba 2.

Simba ina kazi ya kumenyana na JKT Tanzania kesho, Oktoba 4 mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni raundi ya tano.

Inakutana na JKT Tanzania ambayo imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Coastal Union mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao wanaamini kwamba utakuwa na ushindani mkubwa.

Simba yenyewe imetoka kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Gwambina FC mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa. 

Kwenye mchezo wa kesho atakosekana Gerson Fraga ambaye anasumbuliwa na majeraha aliyopata kwenye mchezo wake dhidi ya Biashara United uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo alitumia Fraga alimpisha nyota mzawa Said Ndemla ambaye kwa sasa ameitwa pia kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *