Kigwangalla Aeleza Alivyokuwa Anauza Vitumbua, noreply@blogger.com (Udaku Special)

September 2, 2020

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla, amesema kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliokulia katika mazingira ya kawaida na alikuwa akizunguka mitaa ya Nzega akiuza Vitumbua na jojo.Dkt Kigwangalla ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 2, 2020, Mjini Nzega Mkoani Tabora, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mji huo, wakati mgombea urais wa chama hicho Dkt Magufuli alipopita hapo kunadi sera na kuomba kura kwa wana Nzega.”Mimi nimezaliwa na kukulia katika viunga vya Mji huu ni mtoto wa kawaida kabisa kutoka familia ya kawaida kabisa ya kiswahili, nimezunguka katika Mitaa ya Nzega nikiuza vitumbua na Jojo, nikifanya shughuli za kawaida kabisa ambazo kwa kiasi kikubwa zinafanywa na wananchi ambao siku hizi wanaitwa wanyonge”, amesema Dkt Kigwangalla.Awali Dkt Kigwangalla amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake kwa kumpa nafasi mbalimbali za uongozi Serikalini ikiweno nafasi ya Naibu Waziri wa Afya, pamoja na nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii.,

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Nzega Vijijini na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla, amesema kuwa yeye ni miongoni mwa watu waliokulia katika mazingira ya kawaida na alikuwa akizunguka mitaa ya Nzega akiuza Vitumbua na jojo.

Dkt Kigwangalla ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 2, 2020, Mjini Nzega Mkoani Tabora, alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mji huo, wakati mgombea urais wa chama hicho Dkt Magufuli alipopita hapo kunadi sera na kuomba kura kwa wana Nzega.

“Mimi nimezaliwa na kukulia katika viunga vya Mji huu ni mtoto wa kawaida kabisa kutoka familia ya kawaida kabisa ya kiswahili, nimezunguka katika Mitaa ya Nzega nikiuza vitumbua na Jojo, nikifanya shughuli za kawaida kabisa ambazo kwa kiasi kikubwa zinafanywa na wananchi ambao siku hizi wanaitwa wanyonge”, amesema Dkt Kigwangalla.

Awali Dkt Kigwangalla amemshukuru Rais Magufuli kwa kumuamini katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake kwa kumpa nafasi mbalimbali za uongozi Serikalini ikiweno nafasi ya Naibu Waziri wa Afya, pamoja na nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *