Kesi ya Halima Mdee Yashindwa Kuendelea

October 8, 2020

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini  Dar es salaam, imeahirisha kesi inayomkabili Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA), Halima Mdee, ya kutoa maneno ya kumdhalilisha Rais Dkt.John Magufuli. 

Kesi hiyo ambayo ilikuja kwa ajili ya kuanza utetezi mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba imeshindwa kuendelea baada ya wakili wa Halima Mdee,Peter Kibatala kutokuwepo Mahakamani na kesi hiyo itatajwa tena Novemba 11 mwaka huu.

Aidha upande wa mashtaka uliowakilishwa na wakili wa serikali Grace Mwanga haukua na pingamizi lolote.

Katika kesi ya msingi inadaiwa kuwa Julai 3, 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema, zilizopo mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni, Mdee alitamka maneno dhidi ya Rais John Magufuli kuwa, ‘anaongea hovyo, anatakiwa afungwe breki,’ kitendo kinachodaiwa kuwa ni kumdhalilisha Rais na kusababisha uvunjifu wa amani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *