KENYA: Chama tawala cha Jubilee chatishia kumtimua naibu wa rais, William Ruto

October 3, 2020

Chama tawala cha Jubilee nchini Kenya kimependekeza kuondolewa kwa naibu wa rais Willima Ruto kutoka kwa wadhfa wake kama naibu kiongozi wa chama hicho.

Katibu mkuu wa chama hicho Raphael Tuju amemshutumu bwana Ruto kwa kuwa ‘mjeuri, mwenye madharau na asiyemheshimu Rais Uhuru Kenyatta”.

Taarifa iliosomwa hii leo imezungumzia kuhusu matusi ya hivi karibuni yaliotolewa na wandani wa naibu huyo wa rais yakimlenga mamake Uhuru{ seneta mmoja tayari ameshtakia kwa kutoa matamshi ya chuki} walipokuwa wakimuunga mgombea wao katika uchaguzi wa marudio ambapo chama hicho kilikuwa kimeamua kutowakilishwa mbali na kutokuwepo kwa naibu huyo wa rais katika mkutano wa Jumatatu kuhusu corona wakati abapo rais alilegeza baadhi ya masharti ya kukabiliana na ugonja huo.

Kiti chake kilikuwa kimehifadhiwa katika mkutano huo. Taarifa hiyo inajiri siku moja baada ya naibu huyo wa rais kutembelea makao makuu ya chama hicho na zaidi ya wabunge 35 wanaounga mkono ugombea wake wa urais.

Chama hicho kimeshtumu kwa kujaribu kfanya mapinduzi huku rais akiwa Ufaransa . hapo Jana bwana Ruto alijibu katika mtandao wake wa twitter kwamba ameshangaa kwamba ziara yake ya makao makuu ya cham hicho cha Jubilee ilikuwa habari kuu.

Uongozi wa chama hicho hivi sasa umesema kwamba hautamruhusu kuingia katika makao hayo, ukisema kwamba hautamruhusu kuendesha kampeni zake za urais kutoka katika afisi hiyo ili kuwatishia wapinzani wake.

Lakini wakiongea katika hafla moja mjini Nakuru, Magharibi mwa Kenya, ambayo pia ilihudhuriwa na makamu wa rais William, Ruto, Wabunge kadhaa na maseneta, wamekashifu tangazo hilo la bwana Tuju, huku wakisema kuwa, kama kaimu katibu mkuu wa chama Tuju hana mamlaka hayo na kuwa ofizi za kitaifa za chama ni za wanachama wote.

Bwana Ruto ameanza kufanya kampeni zake za kuwania urais 2022.

Rais Kenyatta amesisitiza kwamba sasa sio muda wa kufanya kampeni na badala yake kutimiza walichoahidi Wakenya.

Hapo jana katika mahojiano na chombo cha habari cha France21, rais Uhuru Kenyatta alikataa kusema iwapo atamuunga mkono William Ruto katika kiny’anga’nyiro cha urais na kusema kuwa lengo lake sasa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *