Kembaki awananga wapinzani “Hawajafanya maendeleo Tarime”, on September 10, 2020 at 10:00 am

September 10, 2020

 Na Timothy Itembe Mara.Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini,Michael Kembaki amesema kuwa kura zilizompa ushindi Esther Matiko ambaye ni mbunge kupitia Chama cha Demkorasia na maendeleo (CHADEMA)ambaye anamaliza mda wake zilikuwa za kukopeshwa kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.Kembaki alisema hayo  kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni kata ya kitare ambapo alisema kuwa Matiko wananchi walimpa Kura za mkopo ili awaletee maendeleo lakini sasa ameshindwa kuwaletea maendeleo sasa wanazidai.”Mimi nitume salamu kwa mbunge wa CHADEMA anayemaliza muda wake akumbuke kuwa kura alizopata ambazo zilimsababisha kutangazwa na kuwa mbunge ajue alikopeshwa na wananchi ili awaletee maendeleo lakini sasa kwasababu ameshindwa kuwaletea maendeleo kura hizo tunazidai,” alisema Kembaki.Kembaki alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa jimbo la Tarime Mjini kumchagua na mgombe urais wa Chama chake John Pombe Magufuli pamoja na wagombea udiwani kupitia  CCM ili kuungana pamoja kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wanananchi wa jimbo la Tarime mjini.Mgombea udiwani kupitia Chama cha mapinduzi kata ya Kitare, Daud Wangwe alisema wananchi wamwamini na kumpa kura kwasababu yeye ni mzoefu wa halmashauri na atahakikisha anawaletea maendeleo wananachi wa kata kitare.Wangwe alisema mwaka 2010 wakati akiwa diwani ndani ya kata ya kitare alifanya maendeleo lakini baada ya kutoka na kukabidhi kijiti hicho kata hiyo ilirudi nyuma kwa maendeleo na sasa kuna haja ya kumurudisha ili aendeleze na kumalizia paliobaki.,

 

Na Timothy Itembe Mara.

Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini,Michael Kembaki amesema kuwa kura zilizompa ushindi Esther Matiko ambaye ni mbunge kupitia Chama cha Demkorasia na maendeleo (CHADEMA)ambaye anamaliza mda wake zilikuwa za kukopeshwa kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

Kembaki alisema hayo  kwenye mkutano wa uzinduzi wa kampeni kata ya kitare ambapo alisema kuwa Matiko wananchi walimpa Kura za mkopo ili awaletee maendeleo lakini sasa ameshindwa kuwaletea maendeleo sasa wanazidai.

“Mimi nitume salamu kwa mbunge wa CHADEMA anayemaliza muda wake akumbuke kuwa kura alizopata ambazo zilimsababisha kutangazwa na kuwa mbunge ajue alikopeshwa na wananchi ili awaletee maendeleo lakini sasa kwasababu ameshindwa kuwaletea maendeleo kura hizo tunazidai,” alisema Kembaki.

Kembaki alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa jimbo la Tarime Mjini kumchagua na mgombe urais wa Chama chake John Pombe Magufuli pamoja na wagombea udiwani kupitia  CCM ili kuungana pamoja kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wanananchi wa jimbo la Tarime mjini.

Mgombea udiwani kupitia Chama cha mapinduzi kata ya Kitare, Daud Wangwe alisema wananchi wamwamini na kumpa kura kwasababu yeye ni mzoefu wa halmashauri na atahakikisha anawaletea maendeleo wananachi wa kata kitare.

Wangwe alisema mwaka 2010 wakati akiwa diwani ndani ya kata ya kitare alifanya maendeleo lakini baada ya kutoka na kukabidhi kijiti hicho kata hiyo ilirudi nyuma kwa maendeleo na sasa kuna haja ya kumurudisha ili aendeleze na kumalizia paliobaki.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *