Kembaki aomba wakina mama kumchagua, on September 17, 2020 at 8:00 am

September 17, 2020

Na Timothy Itembe Mara.Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Michael Kembaki amewaomba wakina mama kumchagua na kuacha kudanganywa na mgombea wa Chama cha Demokeasia na maendeleo CHADEMA,Esther Matiko ambaye wakati akiwa mbunge hakuwaletea maendeleo.Kembaki alisema kuwa wakina mama wamuchague na atawatua ndoo ya maji kichwani kulingana na sera ya maji inavyosema kuwa maji yatapatikana mita 400 kutoka wanapokaa.Kembaki aliongeza kuwa wakina mama wasifanye makosa kama kipindi kilichopita ambapo walimchagua mgombea ubunge wa upinzani na akawaacha kutowafanyia maendeleo na maendeleo yamekwama kuwafikia wakazi wa  jimbo la halmashauri ya Tarime mjini .”Nimekuwa nanyi kwa kila mnachonituma kufanyiwa licha ya kuwa sikuwa mbunge nimetekeleza ahadi nilizoahidi kipindi nagombea licha ya kuwa kura hazikutosha  ili kuwa mbunge nimehudhuria msiba mbalimbali nimechangia makanisa na misikiti kwa hali hiyo mkinichagua yaliyobaki nitatimiza muniamini na kunichagua muone makeke yangu”alisema Kembaki.Kembaki alitumia nafasi hiyo kumuombea kura mgombea urais wa Chama chake,John Pombe Magufuli,mgombea udiwani kata ya Bomani Moseti Gotora ili kwenda kushirikiana katika kuleta maendeleo ndani ya halmashauri ya Tarime mjini.Naye mgombea udiwani kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Bomani,Museti Gotora aliwataka wapiga kura kumwamini licha ya kuwa nikijana wamtume atawaletea maendeleo kwakushirikiana na viongozi wengine akiwemo Kembaki.Gotora aliwaomba wapiga kura kuchagua viongozi wanaotokana na Chama chake cha (CCM) ili kuunda mfumo wa uongozi wa mafiga matatu ndipo maendeleo yatakapowafikia kwa wakati na kuonya kuwa wakichagua kwa kuchanganya maendeleo yatakuja kwa kuchanganya.Kwa upande wake Mairi Wansaku mfanyabiashara wa mafuta ya peterol aliwaomba wananchi wa Tarime mjini kuchagua viongozi wanaotokana na Chama cha mapinduzi ili kujiletea maendeleo huku akimfagilia Rais Magufuli kuwa ametekeleza miradi mingi humu nchini kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.,

Na Timothy Itembe Mara.

Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Michael Kembaki amewaomba wakina mama kumchagua na kuacha kudanganywa na mgombea wa Chama cha Demokeasia na maendeleo CHADEMA,Esther Matiko ambaye wakati akiwa mbunge hakuwaletea maendeleo.

Kembaki alisema kuwa wakina mama wamuchague na atawatua ndoo ya maji kichwani kulingana na sera ya maji inavyosema kuwa maji yatapatikana mita 400 kutoka wanapokaa.

Kembaki aliongeza kuwa wakina mama wasifanye makosa kama kipindi kilichopita ambapo walimchagua mgombea ubunge wa upinzani na akawaacha kutowafanyia maendeleo na maendeleo yamekwama kuwafikia wakazi wa  jimbo la halmashauri ya Tarime mjini .

“Nimekuwa nanyi kwa kila mnachonituma kufanyiwa licha ya kuwa sikuwa mbunge nimetekeleza ahadi nilizoahidi kipindi nagombea licha ya kuwa kura hazikutosha  ili kuwa mbunge nimehudhuria msiba mbalimbali nimechangia makanisa na misikiti kwa hali hiyo mkinichagua yaliyobaki nitatimiza muniamini na kunichagua muone makeke yangu”alisema Kembaki.

Kembaki alitumia nafasi hiyo kumuombea kura mgombea urais wa Chama chake,John Pombe Magufuli,mgombea udiwani kata ya Bomani Moseti Gotora ili kwenda kushirikiana katika kuleta maendeleo ndani ya halmashauri ya Tarime mjini.

Naye mgombea udiwani kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Bomani,Museti Gotora aliwataka wapiga kura kumwamini licha ya kuwa nikijana wamtume atawaletea maendeleo kwakushirikiana na viongozi wengine akiwemo Kembaki.

Gotora aliwaomba wapiga kura kuchagua viongozi wanaotokana na Chama chake cha (CCM) ili kuunda mfumo wa uongozi wa mafiga matatu ndipo maendeleo yatakapowafikia kwa wakati na kuonya kuwa wakichagua kwa kuchanganya maendeleo yatakuja kwa kuchanganya.

Kwa upande wake Mairi Wansaku mfanyabiashara wa mafuta ya peterol aliwaomba wananchi wa Tarime mjini kuchagua viongozi wanaotokana na Chama cha mapinduzi ili kujiletea maendeleo huku akimfagilia Rais Magufuli kuwa ametekeleza miradi mingi humu nchini kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *