Keki hii yazua gumzo, kampuni iliyotengeneza yakiri makosa

September 7, 2020

Shirika la ndege la Uganda limeadhimisha mwaka wake wa kwanza kwa kukata keki ambayo umbo lake limezua gumzo katika mitandao ya kijamii.Air UgandaKampuni iliyooka keki hiyo ilibezwa mitandaoni wikendi iliyopita. Kampuni hiyo imekiri kuwa haikutoa vyema muundo wa ndege ya shirika la ndege la Uganda na kuanzisha shindano la kuoka keki tena hiyo.Katika taarifa yake kampuni ya Britam ambayo inafadhili shindano hilo ilisema:‘’Tulijaribu kutengeza keki ya muundo wa ndege lakini kama mlivyoona kwenye mitandao ya kijamii hatukufanikiwa’’Wito sasa umetolewa kwa waokaji keki wakubwa kwa wadogo kushiriki katika shindano hilo ambalo mshindi atafadhiliwa na kutengeza keki na kupewa nafasi ya kuiwasilisha binafsi kwa shirika la ndege la Uganda.,

Shirika la ndege la Uganda limeadhimisha mwaka wake wa kwanza kwa kukata keki ambayo umbo lake limezua gumzo katika mitandao ya kijamii.

Air UgandaKampuni iliyooka keki hiyo ilibezwa mitandaoni wikendi iliyopita. Kampuni hiyo imekiri kuwa haikutoa vyema muundo wa ndege ya shirika la ndege la Uganda na kuanzisha shindano la kuoka keki tena hiyo.

Katika taarifa yake kampuni ya Britam ambayo inafadhili shindano hilo ilisema:

‘’Tulijaribu kutengeza keki ya muundo wa ndege lakini kama mlivyoona kwenye mitandao ya kijamii hatukufanikiwa’’

Wito sasa umetolewa kwa waokaji keki wakubwa kwa wadogo kushiriki katika shindano hilo ambalo mshindi atafadhiliwa na kutengeza keki na kupewa nafasi ya kuiwasilisha binafsi kwa shirika la ndege la Uganda.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *