Kaze aapa kuanza kwa kishindo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu,

December 29, 2020

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze, ameapa kuanza kwa kishindo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara watakapopambana na Prisons keshokutwa Alhamisi kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.

 
Kaze ambaye amekiongoza kikosi hicho hadi sasa kikiwa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara, amesema anazitaka pointi tatu katika mchezo huo ili kuzidi kuyakaribia malengo yao.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema wakati wakiendelea na maandalizi ya mchezo huo wakiwa jijini Mbeya, Kocha Kaze amekuwa akisisitiza kwamba lazima wauanze mzunguko wa pili na pointi tatu za Prisons.“
Tumejiandaa vema na mechi za mzunguko wa pili chini ya Kocha Kaze ambaye aliwapa mapumziko mafupi wachezaji na sasa tumeingia vitani kwa kufanya mazoezi baada ya sikukuu.
Mazoezi yamefanyika kwa siku tatu katika Uwanja wa JKT Ifunda jijini Mbeya na kesho (leo Jumanne), kikosi kitaelekea Simbawanga mkoani Rukwa kwa ajili ya mchezo.“
Wachezaji wote wapo vizuri, tukiwa kambini Mukoko Tonombe aliugua glafla lakini kwa sasa anaendelea vizuri, alianza mazoezi ya peke yake lakini sasa amejiunga na wenzake.“
Tunafahamu wapinzani wetu Prisons wapo nyumbani, lakini sisi hatujali, tutapambana kuhakikisha tunafanikiwa kupata ushindi mnono,” alisema Bumbuli

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *