Kayumba afunguka kukutwa na taulo kwa Irene Uwoya,

October 10, 2020

Msanii wa BongoFleva Kayumba Asosie amesema Jamhuri ya watu wa mitandao ya kijamii ni wanafki sana kwa sababu wanapenda maneno ndiyo maana wakasababisha kuvunjika kwa ukaribu wake na staa wa filamu hapa nchini Tanzania Irene Uwoya.

Kayumba amezungumza hayo wakati akijibu madai ya kuhusishwa kuwa kwenye mahusiano na Irene Uwoya pamoja na kufumwa akiwa na taulo nyumbani kwa msanii huyo.

“Irene Uwoya alikuwa mshikaji wangu na tukaishia kwenye ushkaji, walivyoanza maneno yao tukaona bora tutulie tusiendelee maana ana familia yake na ana mtoto mkubwa, watu wa mitandaoni wanafki sana sijawahi kukutwa na taulo nyumbani kwake japokuwa nilikuwa naenda sana, halafu mbona ana watu wengi kwanini naonekana mimi tu” msanii Kayumba Asosie

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *