Kayumba Afunguka Kilichokwamisha Jambo lao na IRENE Uwoya….”Ilibaki Kidogo tu’

October 3, 2020

Mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Bongo Star Search (BSS) mwaka 2015 KayumbaJuma, amesema ilibaki kidogo mwigizaji nyota Irene Uwoya awe meneja wake, lakini maneno ya watu yalimkimbiza.

Msanii huyo alisema Uwoya alionesha nia ya kumsimamia kwenye muziki wake ila kutokana na namna walivyokuwa yakaibuka maneno kwenye mitandao ya kijamii kuwa wanatoka pamoja.

“Uwoya alitaka kunisimamia katika muziki wangu kwa hiyo tukaanza kupiga picha na kuweka kwenye mitandao ndipo maneno yakaibuka kuwa tunatoka pamoja na yeye hakuyapenda kwa sababu ni mtu mwenye familia yake hivyo akaamua kuachana na mimi,” alisema Kayumba akizungumza na Wasafi Tv.

Alisema kwa sasa anapambana mwenyewe na meneja wake ingawa bado hajapata uwekezaji wa kutosha kufikisha mbali muziki wake.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *