Katibu UWT Dodoma Mjini atinga kata ya Mihuji kutafuta kura za Dk Magufuli,

October 15, 2020

 

Katibu wa Umoja wa Wanawake Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa ameshiriki kampeni za Udiwani kata ya Miyuji ambapo amemuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini CCM, Anthony Mavunde na Mgombea Udiwani wa Kata hiyo, Beatrice Ngerangera.

Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika mtaa wa Mpamaa, Madukwa amesema miradi ya kimaendeleo iliyofanyika katika Jiji la Dodoma pamoja na kuhamishia serikali jijini Dodoma ni kielelezo cha upendo wa Dk Magufuli kwa wananchi wa jiji hilo na hivyo kuwaomba kujitokeza kwa wingi kumpigia kura nyingi Oktoba 28.

” Mihuji ya miaka mitano nyuma siyo ya leo, Dk Magufuli ametuheshimisha kwa kutuongezea hadhi baada ya kutupa heshima ya kuwa Jiji pamoja na kuhamishia Makao Makuu hapa, wote ni mashahidi jinsi miradi ya kimaendeleo ilivyosukumwa kwenye Jiji letu, ni miradi hiyo imetoa ajira kwa vijana na akina mama wengi, tumuheshimishe na sisi kwa kumpa kura nyingi pamoja na kumletea Mbunge Mavunde na Diwani Beatrice,” Amesema Diana.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *