Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema tuzo ya Nobel ni mshikamano wa kimataifa,

October 9, 2020

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kutolewa kwa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa Shirika la Chakula Duniani – WFP kunaonyesha umuhimu wa mshikamano wa kimataifa. 

Guterres amesema katika taarifa kuwa wahudumu wa WFP huonyesha ujasiri katika mazingira ya hatari ili kuwasilisha bidhaa za kuokoa maisha katika maeneo ya vita na ya majanga. 

Akizungumza wakati akitangaza mshindi wa mwaka huu mjini Oslo, Norway, mwenyekiti wa kamati ya Nobel Berit Reiss-Andersen alisema WFP imepewa tuzo hiyo kwa kuwalisha mamilioni ya watu kutoka Yemen hadi Korea Kaskazini, wakati janga la corona likiwasukuma mamilioni zaidi katika baa la njaa. 

Mkuu wa WFP David Beasley amesema shirika hilo la Umoja wa Mataifa limepokea tuzo hiyo kwa unyenyekevu na heshima kubwa. 

WFP ilianzishwa 1961, na mwaka jana liliwasaidia watu milioni 97 katika nchi 88. 

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, naye pia amelipongeza shirika la WFP kwa kutunukiwa tuzo hiyo, akisema ni kutokana na kutekeleza wajibu mkubwa kwa ubinaadamu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *