Katibu mkuu wa NATO anaitarajia Uturuki kutuliza ghasia Karabakh,

October 5, 2020

 

Katibu mkuu wa jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema leo kuwa anatarajia Uturuki, mshirika wa karibu wa Azerbaijan kutumia ushawishi unaohitajika kutuliza ghasia katika eneo lililojitenga la Nagorno Karabakh linalothibitiwa na Armenia. 

Matamshi ya Stoltenberg yanajiri baada ya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu huku mapigano kati ya vikosi vya Azerbaijan na vile vilivyojitenga vya Armenia yakiingia wiki yake ya pili na kusababisha vifo vya takriban watu 250.

Stoltenberg amesema kuwa wanasikitishwa na kuongezeka kwa uhasama huo. Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alikuwa ameihimiza Azerbaijan kuendeleza mashambulizi yake hadi itakapotwaa ardhi yake iliyopoteza katika vita vya miaka ya mwanzo ya 1990 vilivyosababisha vifo vya watu elfu 30 wakati muungano wa zamani wa Sovieti uliposambaratika.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *