Kassinge ataja mambo atakayoanza kushughulikia, on September 15, 2020 at 6:00 pm

September 15, 2020

 Na Ahmad Mmow, Lindi.Mgombea ubunge wa jimbo la Kilwa Kusini kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Ally Kassinge ameahidi atasimamia kikamilifu upatikanaji wa maji, ajira, bei za mazo ya kilimo na miundombinu ya barabara iwapo atachuguliwa na kuwa mbunge wa jimbo hilo.Kassinge ametoa ahadi hiyo kwanyakati na maeneo tofauti katika vijiji vya Pande Mikoma, Mavuji na Mchama kupitia mikutano ya kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo.Kassinge alisema jimbo hilo linachangamoto nyingi ambazo zinatatulika iwapo wananchi watamchagua mwakilishi mbunifu anayetokana na chama makini chenye ilani inayotekelezeka kwa vitendo. Ambapo katika uchaguzi wa mwaka huu mwakilishi makini ni yeye, na chama chenye ilani inayotekelezeka kwa vitendo ni ilani ya CCM ambayo imegusa kila sekta.Alisema licha ya changamoto nyingi zilizopo katika jimbo hilo amezitazama sekta za maji, bararabara, kilimo na,uvuvi  kilimo amebaini kwamba zinatakiwa kutatuliwa haraka na ndizo atakazo anza kushughulika nazo iwapo wapiga kura watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao.Alisema tatizo la maji limegeuka kuwa sugu katika maeneo mengi jimboni humo. Ingawa mbunge aliyemaliza muda wake alikuwa mbunge kwa vipindi viwili. Lakini kutokana nakutokuwa mbunifu na dhamira ya kweli ya kuondoa tatizo hilo ameshindwa. Hatahivyo yeye atamaliza tatizo hilo.Alisema ni jambo lisilokubalika kuona wananchi wa jimbo hilo wanahangaika kutafuta maji kiasi cha kutembea umbali mrefu kufuata maji wakati wilaya ya Kilwa ikiwamo jimbo la Kilwa Kusini ina vyanzo vingi vya maji.Ikiwa ni pamoja na chanzo cha maji cha mto Mavuji.Kuhusu kilimo, Kassinge alisema ni CCM pekee ndicho chenye uwezo wakuwatetea wakulima na kuwapa maslahi mazuri yanayotokana na kazi wanazofanya. Akiahidi yeye atahakikisha mazao ya wakulima yanakuwa na bei nzuri. Kwani ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 imeeleza kwakina jinsi ya kuboresha sekta ya kilimo na maslahi ya wakulima.Alibainisha kwamba kasoro ambazo zilionekana kuwa ni kikwazo cha kufanikisha azima njema ya serikali ya kuanzisha ununuzi wa mazao kwakutumia stakabadhi za maghala( stakabadhi ghalani) zimerekebishwa. Kwahiyo atahakikisha anasimamia vema sekta hiyo ili wakulima wapate bei nzuri.Aidha mgombea huyo aliitaja miundo mbinu ya barabara ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi kuwa ni changamoto. Kwani barabara nyingi kipindi cha masika zinapitika kwa shida. Akiitaja barabara za Hoteli tatu- Pande, Mkazambo- Lihimalyao kuwa ni miongoni kwa barabara hizo.Kwakuzingatia ukweli huo, alisema akichaguliwa nakuwa mbunge atahakikisha barabara hizo zinafanyiwa matengenezo ya uhakika ili wananchi waweze kusafiri muda waote bila usumbufu. Nikutokana na kuamini kwamba bila barabara za uhakika hakuna maendeleo.Kuhusu sekta ya uvuvi alisema licha yakwamba asilimia sabini ya watu wanaoishi katika ukanda wa Pwani kazi yao inayowaingizia kipato ni uvuvi, lakini bado hawajanufaika na kazi hiyo. Nikutokana na wavuvi kutowezeshwa. Hali inayosababisha wavue kwakutumia zana duni. ” Nikiwa mbunge wenu nitashughulikia changamoto zilizopo kwenye sekta ya uvuvi. Kilwa ina maliasili za misitu, bahari, misitu na ardhi. Lakini pia tuna madini na gesi ambazo zote hizo zikisimamiwa vizuri zinafursa ambazo zikitumiwa vizuri tunaweza kuondokana na umaskini. Kilichokosekana kwa miaka mingi ni mwakilishi mwenye maono na mbunifu tu,” alisisitiza Kassinge.Aliahidi kwamba atahakikisha mazao ya kilimo, bahari na uvuvi yanaongezewa thamani ndani ya wilaya hiyo kwakusimamia, kuhamasisha na kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao ya misitu, kusindika samaki na kusindika mazao ya kilimo.  Kwani licha ya kuongeza thamani ya mazao hayo, lakini pia viwanda hivyo vitatoa ajira za moja kwa moja na ajira mbadala.Katika hali inayoonesha Kassinge amedhamiria kufanya mengi na anakiu ya kutatua changamoto zilizopo katika jimbo hilo alisema iwapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge atashirikiana na serikali kwa ukaribu ili kuhakikisha migogoro ya ardhi inakwisha.Alisema migogoro ya ardhi nikwazo kwa maendeleo ya wananchi. Kwahiyo atasimamia mpango wa matumizi  bora ya ardhi, wananchi wapimiwe maeneo yao na wapate hati za kumiliki maeneo hayo. Huku akiwahakikishia wananchi hao kwamba yote hayo yanawezekana.” Zipo zahanati ambazo ujenzi wake umesimama kwa muda mrefu. Hali inayosababisha wananchi kutembea umbali mrefu kufuata matibabu na huduma nyingine za afya. Nikiwa Mbunge wenu nawahakikishia ninasimamia na kuisukuma serikali zikamilike haraka,” alisema Kassinge.Kwaupande wake mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kilwa, Kambi Mandai alisema wananchi wa jimbo hilo wabadilike kwa kumchagua mbunge atakaye kwenda na hoja bungeni badala ya vioja. Kwamadai kwamba kwakipindi cha miaka kumi jimbo hilo lilikuwa na mbunge mchekeshaji badala ya msemaji.Nae katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mayasa Kimbau alitoa wito kwa wapiga kura wamchague mgombea huyo ambaye atatumia uzoefu wa uongozi aliopata akiwa serikalini kwa nafasi za ukurugenzi wa halmashauri na ukuu wa wilaya kutatua changamoto zilizopo katika jimbo hilo la Kilwa Kusini.,

 

Na Ahmad Mmow, Lindi.

Mgombea ubunge wa jimbo la Kilwa Kusini kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Ally Kassinge ameahidi atasimamia kikamilifu upatikanaji wa maji, ajira, bei za mazo ya kilimo na miundombinu ya barabara iwapo atachuguliwa na kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Kassinge ametoa ahadi hiyo kwanyakati na maeneo tofauti katika vijiji vya Pande Mikoma, Mavuji na Mchama kupitia mikutano ya kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo.

Kassinge alisema jimbo hilo linachangamoto nyingi ambazo zinatatulika iwapo wananchi watamchagua mwakilishi mbunifu anayetokana na chama makini chenye ilani inayotekelezeka kwa vitendo. Ambapo katika uchaguzi wa mwaka huu mwakilishi makini ni yeye, na chama chenye ilani inayotekelezeka kwa vitendo ni ilani ya CCM ambayo imegusa kila sekta.

Alisema licha ya changamoto nyingi zilizopo katika jimbo hilo amezitazama sekta za maji, bararabara, kilimo na,uvuvi  kilimo amebaini kwamba zinatakiwa kutatuliwa haraka na ndizo atakazo anza kushughulika nazo iwapo wapiga kura watampa ridhaa ya kuwa mbunge wao.

Alisema tatizo la maji limegeuka kuwa sugu katika maeneo mengi jimboni humo. Ingawa mbunge aliyemaliza muda wake alikuwa mbunge kwa vipindi viwili. Lakini kutokana nakutokuwa mbunifu na dhamira ya kweli ya kuondoa tatizo hilo ameshindwa. Hatahivyo yeye atamaliza tatizo hilo.

Alisema ni jambo lisilokubalika kuona wananchi wa jimbo hilo wanahangaika kutafuta maji kiasi cha kutembea umbali mrefu kufuata maji wakati wilaya ya Kilwa ikiwamo jimbo la Kilwa Kusini ina vyanzo vingi vya maji.Ikiwa ni pamoja na chanzo cha maji cha mto Mavuji.

Kuhusu kilimo, Kassinge alisema ni CCM pekee ndicho chenye uwezo wakuwatetea wakulima na kuwapa maslahi mazuri yanayotokana na kazi wanazofanya. Akiahidi yeye atahakikisha mazao ya wakulima yanakuwa na bei nzuri. Kwani ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 imeeleza kwakina jinsi ya kuboresha sekta ya kilimo na maslahi ya wakulima.

Alibainisha kwamba kasoro ambazo zilionekana kuwa ni kikwazo cha kufanikisha azima njema ya serikali ya kuanzisha ununuzi wa mazao kwakutumia stakabadhi za maghala( stakabadhi ghalani) zimerekebishwa. Kwahiyo atahakikisha anasimamia vema sekta hiyo ili wakulima wapate bei nzuri.

Aidha mgombea huyo aliitaja miundo mbinu ya barabara ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi kuwa ni changamoto. Kwani barabara nyingi kipindi cha masika zinapitika kwa shida. Akiitaja barabara za Hoteli tatu- Pande, Mkazambo- Lihimalyao kuwa ni miongoni kwa barabara hizo.

Kwakuzingatia ukweli huo, alisema akichaguliwa nakuwa mbunge atahakikisha barabara hizo zinafanyiwa matengenezo ya uhakika ili wananchi waweze kusafiri muda waote bila usumbufu. Nikutokana na kuamini kwamba bila barabara za uhakika hakuna maendeleo.

Kuhusu sekta ya uvuvi alisema licha yakwamba asilimia sabini ya watu wanaoishi katika ukanda wa Pwani kazi yao inayowaingizia kipato ni uvuvi, lakini bado hawajanufaika na kazi hiyo. Nikutokana na wavuvi kutowezeshwa. Hali inayosababisha wavue kwakutumia zana duni. 

” Nikiwa mbunge wenu nitashughulikia changamoto zilizopo kwenye sekta ya uvuvi. Kilwa ina maliasili za misitu, bahari, misitu na ardhi. Lakini pia tuna madini na gesi ambazo zote hizo zikisimamiwa vizuri zinafursa ambazo zikitumiwa vizuri tunaweza kuondokana na umaskini. Kilichokosekana kwa miaka mingi ni mwakilishi mwenye maono na mbunifu tu,” alisisitiza Kassinge.

Aliahidi kwamba atahakikisha mazao ya kilimo, bahari na uvuvi yanaongezewa thamani ndani ya wilaya hiyo kwakusimamia, kuhamasisha na kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao ya misitu, kusindika samaki na kusindika mazao ya kilimo.  Kwani licha ya kuongeza thamani ya mazao hayo, lakini pia viwanda hivyo vitatoa ajira za moja kwa moja na ajira mbadala.

Katika hali inayoonesha Kassinge amedhamiria kufanya mengi na anakiu ya kutatua changamoto zilizopo katika jimbo hilo alisema iwapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge atashirikiana na serikali kwa ukaribu ili kuhakikisha migogoro ya ardhi inakwisha.

Alisema migogoro ya ardhi nikwazo kwa maendeleo ya wananchi. Kwahiyo atasimamia mpango wa matumizi  bora ya ardhi, wananchi wapimiwe maeneo yao na wapate hati za kumiliki maeneo hayo. Huku akiwahakikishia wananchi hao kwamba yote hayo yanawezekana.

” Zipo zahanati ambazo ujenzi wake umesimama kwa muda mrefu. Hali inayosababisha wananchi kutembea umbali mrefu kufuata matibabu na huduma nyingine za afya. Nikiwa Mbunge wenu nawahakikishia ninasimamia na kuisukuma serikali zikamilike haraka,” alisema Kassinge.

Kwaupande wake mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Kilwa, Kambi Mandai alisema wananchi wa jimbo hilo wabadilike kwa kumchagua mbunge atakaye kwenda na hoja bungeni badala ya vioja. Kwamadai kwamba kwakipindi cha miaka kumi jimbo hilo lilikuwa na mbunge mchekeshaji badala ya msemaji.

Nae katibu wa CCM wa wilaya hiyo, Mayasa Kimbau alitoa wito kwa wapiga kura wamchague mgombea huyo ambaye atatumia uzoefu wa uongozi aliopata akiwa serikalini kwa nafasi za ukurugenzi wa halmashauri na ukuu wa wilaya kutatua changamoto zilizopo katika jimbo hilo la Kilwa Kusini.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *