Kanye West akwama kuwania Urais Marekani

September 15, 2020

Nyota wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kany West, ameshindwa kufuzu kuwa mmoja kati ya wagombea wa urais katika mji wa Wisconsin kutokana na kuchelewa kuwasilisha nyaraka zake kwa wakati.Maamuzi hayo yalifanywa na Jaji wa Mahakama ya Brown County Circuit, John Zakowski ambapo alimuondoa msanii huyo kwenye Tume ya Uchaguzi ya Wisconsin.Msanii huyo alitakiwa kupeleka nyaraka hizo kabla ya Agosti 4 saa 11 jioni, lakini yeye alifika kwenye ofisi hizo saa 11 na sekunde 14, wakati huo tayari mfumo wa upokeaji nyaraka umesimama.Hata hivyo Kanye West alikata rufaa, lakini Ijumaa wiki iliopita ilisikilizwa rufaa yake ila bado iligonga mwamba. Kanye West anaamini mwisho wa kuwasilisha nyaraka hizo ilitakiwa kuwa saa 11:01 na sio kamili.,

Nyota wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kany West, ameshindwa kufuzu kuwa mmoja kati ya wagombea wa urais katika mji wa Wisconsin kutokana na kuchelewa kuwasilisha nyaraka zake kwa wakati.

Maamuzi hayo yalifanywa na Jaji wa Mahakama ya Brown County Circuit, John Zakowski ambapo alimuondoa msanii huyo kwenye Tume ya Uchaguzi ya Wisconsin.

Msanii huyo alitakiwa kupeleka nyaraka hizo kabla ya Agosti 4 saa 11 jioni, lakini yeye alifika kwenye ofisi hizo saa 11 na sekunde 14, wakati huo tayari mfumo wa upokeaji nyaraka umesimama.

Hata hivyo Kanye West alikata rufaa, lakini Ijumaa wiki iliopita ilisikilizwa rufaa yake ila bado iligonga mwamba. Kanye West anaamini mwisho wa kuwasilisha nyaraka hizo ilitakiwa kuwa saa 11:01 na sio kamili.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *