Kansela Angela Merkel haondowi uwezekano wa kuzuia mradi wa bomba la gesi Urusi, on September 7, 2020 at 6:00 pm

September 7, 2020

Msemaji mkuu wa Kansela Angela Merkel, Steffen Seibert amesema kiongozi huyo wa Ujerumani haondowi uwezekano wa kuzuia mradi wa bomba la gesi wa Nord Stream 2, kama hatua ya kuijibu Urusi katika kisa cha kupewa sumu mkosoaji wa serikali hiyo ya Urusi.Mradi huo wa bomba la gesi ulikusudiwa kusafirisha gesi kutoka Urusi hadi Ujerumani. Seibert amesema kwamba Kansela Merkel ana mtazamo sawa na maelezo yaliyotolewa na waziri wake wa mambo ya nje Heiko Maas.Waziri Maas jana Jumapili akihojiwa alisema hatua itakayochukuliwa na Urusi ndiyo itakayoamua ikiwa Ujerumani itabadilisha msimamo wake wa muda mrefu wa kuunga mkono mradi huo wa bomba la gesi la Nord Stream 2.Awali kansela Merkel alisisitiza juu ya kutenganisha kisa cha Navalny na mradi huo unaopingwa vikali na Marekani.,

Msemaji mkuu wa Kansela Angela Merkel, Steffen Seibert amesema kiongozi huyo wa Ujerumani haondowi uwezekano wa kuzuia mradi wa bomba la gesi wa Nord Stream 2, kama hatua ya kuijibu Urusi katika kisa cha kupewa sumu mkosoaji wa serikali hiyo ya Urusi.

Mradi huo wa bomba la gesi ulikusudiwa kusafirisha gesi kutoka Urusi hadi Ujerumani. Seibert amesema kwamba Kansela Merkel ana mtazamo sawa na maelezo yaliyotolewa na waziri wake wa mambo ya nje Heiko Maas.

Waziri Maas jana Jumapili akihojiwa alisema hatua itakayochukuliwa na Urusi ndiyo itakayoamua ikiwa Ujerumani itabadilisha msimamo wake wa muda mrefu wa kuunga mkono mradi huo wa bomba la gesi la Nord Stream 2.

Awali kansela Merkel alisisitiza juu ya kutenganisha kisa cha Navalny na mradi huo unaopingwa vikali na Marekani.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *