Kamati yashindwa kuamua kesi ya Morrison,

October 13, 2020

 Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF), imeshindwa kujadili shauri la mchezaji Bernard Morrison wa Simba SC, baada ya mchezaji huyo kushindwa kufika mbele ya kamati hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Mwita Kichere Waissaka, amesema kamati haikujadili shitaka la Bernard Morrison kwa sababu mlalamikiwa hakufika mbele ya kamati na alitoa udhuru kuwa yupo kwenye michezo ya klabu yake ya Simba SC, lakini alituma wawakilishi.

Kutokana na unyeti wa shauri hilo Mwenyekiti Kichere amesema ni muhimu sana mlalamikiwa awepo mwenyewe, ili haki iweze kutendeka kwa sababu kuna maswali ambayo wawakilishi hawawezi kujibu kwa hiyo swala lake liliahirishwa.

Bernard Morrison alifikishwa mbele ya kamati ya maadili na kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba na klabu ya Simba SC, huku akiwa na kesi ya uhalali wa mkataba wake na klabu yake ya zamani ya Yanga ndani ya shirikisho hilo.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *