Kamala Harris anatembelea Vietnam na Singapore mwezi huu

August 4, 2021

Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris atalenga katika kutetea kanuni za kimataifa katika bahari ya South China, kuimarisha uongozi wa kieneo wa Marekani na kupanua ushirikiano wa usalama, wakati wa ziara yake ya Vietnam na Singapore mwezi huu afisa mwandamizi wa White House aliliambia shirika la Habari la Reuters.

Harris atakuwa Makamu Rais wa kwanza wa Marekani kutembelea Vietnam, wakati Washington inataka kuimarisha msaada wa kimataifa kukabiliana na ushawishi wa China unaokuwa ulimwenguni.

Kamala Harris, Makamu Rais wa Marekani

Kamala Harris, Makamu Rais wa Marekani

Afisa huyo wa Marekani alisema Washington inaziona nchi zote mbili kama marafiki muhimu kutokana na maeneo yao, ukubwa wa uchumi wao, uhusiano wa kibiashara na usalama juu ya masuala kama vile bahari ya South China, ambayo China inadai ni eneo lake.

Adui wa zamani wa Marekani, Vietnam, amekuwa mpinzani mkubwa wa madai ya China kuhuhu bahari ya South China. Nchi katika eneo hilo zinakaribisha kwa kiasi kikubwa uwepo wa jeshi la Marekani, katika kukabiliana na walinzi wa pwani na shughuli za uvuvi za China.

Source link

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *