Kagere Aitaka Tena Rekodi Ya Mabao Simba

September 8, 2020

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere, amefichua kuwa bado ana ndoto kubwa ya kuendelea kufunga mabao katika Ligi Kuu Bara msimu huu, licha ya kuwepo kwa ushindani wa namba.Mshambuliaji huyo amefanikiwa kuibuka mfungaji bora mara mbili mfululizo baada ya msimu wake wa kwanza kufunga mabao 23 kabla ya msimu uliopita kufunga mabao 22 katika Ligi Kuu Bara akifuatiwa na mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mtanzania, Yusuph Mhilu ambaye alifunga mabao 13 sawa na Wazir Junior aliyekuwa Mbao kabla ya kutua Yanga msimu huu.Akizungumza na Championi Jumatatu, Kagere alisema kuwa anachokiangalia kwa sasa ni kuona anaweza kufikia rekodi yake ya msimu uliopita katika ligi ya msimu huu, licha ya kuamini kuwepo kwa ushandani mkali kutoka kwa washambuliaji wengine.“Kitu kikubwa kwa sasa ni kujitoa kwangu katika kuisaidia timu kwa kuhakikisha inapata matokeo katika kila mchezo ambao tunacheza kwa sababu ligi tayari imeshaanza, hilo ndiyo jambo muhimu kwa sasa.“Natamani kuona nafikia rekodi yangu ya mabao kwa sababu ndiyo itasaidia katika timu kupata mafanikio ya kutetea ubingwa, ingawa kila mchezaji hapa anaweza kufunga lakini kwangu nitahakikisha kila nafasi nitakayoweza kucheza basi niwe nafunga ili kuisaidia timu pamoja na kufikia malengo,” alisema Kagere,

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mnyarwanda, Meddie Kagere, amefichua kuwa bado ana ndoto kubwa ya kuendelea kufunga mabao katika Ligi Kuu Bara msimu huu, licha ya kuwepo kwa ushindani wa namba.

Mshambuliaji huyo amefanikiwa kuibuka mfungaji bora mara mbili mfululizo baada ya msimu wake wa kwanza kufunga mabao 23 kabla ya msimu uliopita kufunga mabao 22 katika Ligi Kuu Bara akifuatiwa na mshambuliaji wa Kagera Sugar, Mtanzania, Yusuph Mhilu ambaye alifunga mabao 13 sawa na Wazir Junior aliyekuwa Mbao kabla ya kutua Yanga msimu huu.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kagere alisema kuwa anachokiangalia kwa sasa ni kuona anaweza kufikia rekodi yake ya msimu uliopita katika ligi ya msimu huu, licha ya kuamini kuwepo kwa ushandani mkali kutoka kwa washambuliaji wengine.

“Kitu kikubwa kwa sasa ni kujitoa kwangu katika kuisaidia timu kwa kuhakikisha inapata matokeo katika kila mchezo ambao tunacheza kwa sababu ligi tayari imeshaanza, hilo ndiyo jambo muhimu kwa sasa.

“Natamani kuona nafikia rekodi yangu ya mabao kwa sababu ndiyo itasaidia katika timu kupata mafanikio ya kutetea ubingwa, ingawa kila mchezaji hapa anaweza kufunga lakini kwangu nitahakikisha kila nafasi nitakayoweza kucheza basi niwe nafunga ili kuisaidia timu pamoja na kufikia malengo,” alisema Kagere

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *