Jumuiya ya kujihami ya NATO kujadili suala la kupewa sumu Navalny, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 4, 2020 at 1:00 pm

September 4, 2020

Tukio la kupewa sumu kwa Alexei Navalny litajadiliwa katika mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO hii leo baada ya viongozi wa Ulaya kutishia kuiwekea Urusi vikwazo vipya. Urusi imekanusha vikali madai hayo ya kumpa sumu kiongozi huyo wa upinzani. Viongozi wa Magharibi wametaka majibu kutoka kwa Urusi baada ya Ujerumani kusema kuna ushahidi wa kutosha kwamba wakili huyo mwenye umri wa miaka 44 alipewa sumu ya Novichok. Ni sumu sawia na hiyo iliyotumika kwa jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na mwanawe wa kike katika mji wa Salisbury huko Uingereza. Ujerumani itatoa taarifa mbele ya kikao cha NATO leo huko mjini Brussels kisha Katibu Mkuu Jens Stoltenberg atazungumza na vyombo vya habari baadae.,

Tukio la kupewa sumu kwa Alexei Navalny litajadiliwa katika mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO hii leo baada ya viongozi wa Ulaya kutishia kuiwekea Urusi vikwazo vipya.

 Urusi imekanusha vikali madai hayo ya kumpa sumu kiongozi huyo wa upinzani. Viongozi wa Magharibi wametaka majibu kutoka kwa Urusi baada ya Ujerumani kusema kuna ushahidi wa kutosha kwamba wakili huyo mwenye umri wa miaka 44 alipewa sumu ya Novichok. 

Ni sumu sawia na hiyo iliyotumika kwa jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na mwanawe wa kike katika mji wa Salisbury huko Uingereza. 

Ujerumani itatoa taarifa mbele ya kikao cha NATO leo huko mjini Brussels kisha Katibu Mkuu Jens Stoltenberg atazungumza na vyombo vya habari baadae.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *