John Legend na mkewe wapata pigo baada ya kufiwa na mtoto wao,

October 1, 2020

Familia ya Mwanamuziki maarufu duniani John Legend aliyetamba na wimbo wa “All of You” wamepata pigo baada ya kumpoteza mtoto wao waliyemtegemea kumpata.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa mke wa John Legend, Chrissy Teigen ameandika ujumbe mzito kuhusu kutokea kwa tatizo la kumpoteza mtoto waliyetegemea kumpata.

Chrissy Teigen ameeleza kuwa sababu pekee iliyosababisha mtoto wao kufariki ni baada yakuvuja damu nyingi kitendo ambacho kimefanya jambo hilo kutokea.

Hata hivyo amewashukuru wote ambao wamekuwa naye pamoja katika kipindi hiki kigumu akiwemo mwanamitindo maarufu duniani #KimKardashian ambaye amekuwa naye pamoja mwanzo mpaka mwisho katika hali yake.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *