Joe Biden asema kupigwa risasi Jacob Blake kunaweza kuisaidia marekani kupambana na ubaguzi, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 4, 2020 at 1:00 pm

September 4, 2020

Mgombea wa urais nchini Marekani kupitia chama cha Democratic Joe Biden hapo jana alifanya ziara katika mji wenye mivutano wa Kenosha, na kutoa ujumbe ambao unatofautiana pakubwa na mtazamo wa Rais Donald Trump mnamo wakati matukio ya ghasia yakizusha hamasa kubwa nchini Marekani. Katika ujumbe huo Biden amesema ghasia zilizofuatia kitendo cha polisi kumpiga risasi mwanamme mweusi, Jacob Blake katika mjini huo, kinaweza kuisaidia Marekani kutafakari mfumo wake wa ubaguzi wa rangi uliodumu kwa karne kadhaa. “Maneno ya rais ni muhimu, haijalishi kama ni mazuri, mabaya au tofauti, ni muhimu. Haijalishi kama rais anaijua au haijui kazi yake, maneno yake yanaweza kuiingiza nchi katika vita. Maneno hayo yanaweza kuleta amani pia. Yanaweza kufanya masoko yakainuka na kuanguka na yanaweza kuleta tofauti kwa jinsi tu wanavyoyasema.”Huku Biden akiwa alijumuika na familia ya Blake kwa zaidi ya saa moja, Trump hakuitembelea familia hiyo katika ziara yake juzi. Wakati ambapo Biden amesema kuwa matatizo ya ubaguzi wa rangi yalianzia enzi za utumwa huko Marekani, Trump alikataa kukiri kwamba kuna ubaguzi wa rangi na akawaunga mkono maafisa wa usalama akisema machafuko mjini humo yametokana na kile alichokiita “ugaidi wa ndani ya nchi.”,

Mgombea wa urais nchini Marekani kupitia chama cha Democratic Joe Biden hapo jana alifanya ziara katika mji wenye mivutano wa Kenosha, na kutoa ujumbe ambao unatofautiana pakubwa na mtazamo wa Rais Donald Trump mnamo wakati matukio ya ghasia yakizusha hamasa kubwa nchini Marekani. 

Katika ujumbe huo Biden amesema ghasia zilizofuatia kitendo cha polisi kumpiga risasi mwanamme mweusi, Jacob Blake katika mjini huo, kinaweza kuisaidia Marekani kutafakari mfumo wake wa ubaguzi wa rangi uliodumu kwa karne kadhaa. 

“Maneno ya rais ni muhimu, haijalishi kama ni mazuri, mabaya au tofauti, ni muhimu. Haijalishi kama rais anaijua au haijui kazi yake, maneno yake yanaweza kuiingiza nchi katika vita. 

Maneno hayo yanaweza kuleta amani pia. 

Yanaweza kufanya masoko yakainuka na kuanguka na yanaweza kuleta tofauti kwa jinsi tu wanavyoyasema.

“Huku Biden akiwa alijumuika na familia ya Blake kwa zaidi ya saa moja, Trump hakuitembelea familia hiyo katika ziara yake juzi.

 Wakati ambapo Biden amesema kuwa matatizo ya ubaguzi wa rangi yalianzia enzi za utumwa huko Marekani, Trump alikataa kukiri kwamba kuna ubaguzi wa rangi na akawaunga mkono maafisa wa usalama akisema machafuko mjini humo yametokana na kile alichokiita “ugaidi wa ndani ya nchi.”

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *