Joe Biden aionya Uingereza kuhusu Brexit, on September 17, 2020 at 1:00 pm

September 17, 2020

Mgombea urais wa Marekani Joe Biden ameionya Uingereza kwamba inapaswa kuyaheshimu makubaliano ya amani ya Ireland Kaskazini katika wakati ambapo nchi hiyo inajiondowa katika Umoja wa Ulaya au haitofanikiwa kuwa na makubaliano ya kibiashara na Marekani.Kupitia ujumbe wa Twitta mgombea huyo wa urais kupitia chama cha Democratic,amesema hawawezi kuruhusu makubaliano ya Ijumaa kuu,yaliyosababisha kupatikana amani Ireland Kaskazini kuwa muhanga wa mpango wa Brexit. Onyo la Biden limekuja wakat waziri mkuu wa Uingereza ametangaza sheria itakayofuta sehemu ya makubaliano ya Brexit inayohusiana na suala la Ireland Kaskazini. Johnson anaulaumu Umoja wa Ulaya kwa kutaka kuyavuruga mazungumzo ya kibiashara na kujaribu kuigawa Uingereza.Umoja wa Ulaya unasema kukiukwa kwa namna yoyote makubaliano ya Brexit kunaweza kukazamisha mazungumzo ya kibiashara na hivyo kusababisha hali ngumu kwenye mpaka kati ya Ireland Kaskazini na Ireland ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.,

Mgombea urais wa Marekani Joe Biden ameionya Uingereza kwamba inapaswa kuyaheshimu makubaliano ya amani ya Ireland Kaskazini katika wakati ambapo nchi hiyo inajiondowa katika Umoja wa Ulaya au haitofanikiwa kuwa na makubaliano ya kibiashara na Marekani.Kupitia ujumbe wa Twitta mgombea huyo wa urais kupitia chama cha Democratic,amesema hawawezi kuruhusu makubaliano ya Ijumaa kuu,yaliyosababisha kupatikana amani Ireland Kaskazini kuwa muhanga wa mpango wa Brexit. 

Onyo la Biden limekuja wakat waziri mkuu wa Uingereza ametangaza sheria itakayofuta sehemu ya makubaliano ya Brexit inayohusiana na suala la Ireland Kaskazini. 

Johnson anaulaumu Umoja wa Ulaya kwa kutaka kuyavuruga mazungumzo ya kibiashara na kujaribu kuigawa Uingereza.Umoja wa Ulaya unasema kukiukwa kwa namna yoyote makubaliano ya Brexit kunaweza kukazamisha mazungumzo ya kibiashara na hivyo kusababisha hali ngumu kwenye mpaka kati ya Ireland Kaskazini na Ireland ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *