Jinsi wanahabari wanavyoshambuliwa Nigeria

September 8, 2020

Dakika 3 zilizopita

Former Nigerian minister Femi Fani-Kayode at the Calabar press conference in August 2020

Maelezo ya picha,

Waziri wa zamani wa Nigeria, Femi Fani-Kayode

Katika mfululizo wa barua kutoka kwa waandishi wa habari wa Afrika, Mannir Dan Ali, mhariri mkuu wa zamani wa gazeti la Daily Trust, anaangazia changamoto zinazowakabili wanahabari wa Nigeria kwa sababu tu ya kutekeleza kazi zao.

Maswali nchini Nigeria bado yanaulizwa kuhusu kwanini maafisa wanawatazama wanahabari kama wavulana wadogo.

Hii ni baada ya ghadhabu zilizojitokeza baada ya mwanahabari mmoja kukutana na maneno mabaya kutoka kwa waziri wa zamani wa serikali na mfuasi wa chama cha upinzani cha People’s Democratic Party (PDP).

Yote hayo yalinaswa kwenye video, pale Femi Fani-Kayode alipoonesha kutolifurahia swali aliloulizwa na mwandishi wa habari Eyo Charles.

Bwana Fani-Kayode ambaye hana nafasi yoyote anayoishikilia serikalini au katika chama cha PDP, amekuwa akikagua miradi ya serikali nchi nzima

Quote card: Eyo Charles unfinished question to Femi Fani-Kayode: "Sir, please you did not disclose to us who is bankrolling you…"

Kila baada ya ukaguzi, huwaita wanahabari na kupongeza na kuipitisha miradi hiyo.

Ilikuwa katika jimbo la Calabar, jimbo la tatu kulipitia katika miezi ya karibuni, ambapo Bwana Fani-Kayode, alipopandwa na jazba baada ya Charles kuuliza kuhusu gharama za safari zake:

”Mheshimiwa, tafadhali hujatuweka wazi ni nani anayekufadhili..”

Badala hata ya kumruhusu mwandishi wa habari amalize swali lake, Bwana Fani-Kayode alifura na kumuita ”mpumbavu” na kudai kuwa mwandishi huyo alikuwa anaonekana kama mwanaume fukara aliyekusanya rushwa, hapa inajulikana kama ”bahasha” kutoka kwa watu wanaotengeneza habari.

Mimi halikadhalika nilishawahi kukabiliwa naye , alipokuwa serikalini akihudumu kwenye baraza la Rais wa zamani Olesegun Obasanjo zaidi ya miaka kumi iliyopita.

Nilichokipata ni zaidi ya tusi. Ilikuwa katika eneo moja liitwalo Aso Rock , ambapo alitishia kuninasa kibao, hali iliyosababisha mtafaruku na wanahabari kuingilia kati kuondosha shari.

Sikujua wakati ule kwa nini alikuwa na hasira; ni baadae tu, nilielewa ilikuwa ni maoni tata aliyoyatoa kwenye mahojiano ya moja kwa moja na BBC kuhusu mipango ya bwana Obasanjo kuwania muhula wa tatu.

Mahojiano hayo yaligeuka kuwa habari motomoto kisha hasira zake akazihamishia kwangu mwandishi wa habari wa BBC .

Mjeledi wa Farasi

Si tu Bwana Fani-Kayode anayewaona wanahabari kama watu wanaokera.

Miezi kadhaa nyuma, gavana wa jimbo la Kusini-Mashariki Ebonyi aliwapiga marufuku waandishi wawili kufanya kazi katika eneo hilo kwa kile alichodai ni kuripoti mambo mabaya kuhusu jimbo hilo.

”Kama unafikiri una kalamu, tuna koboko”, gavana alionya akitumia neno la kienyeji kwa maana ya mjeledi wa farasi”.

2px presentational grey line

Mjadala kuhusu suala hilo kutoka kwa vyombo vya habari kulimfanya gavana kutengua adhabu .

Miaka kadhaa iliyopita, katika gazeti la Daily Trust, tulilazimika kumuondoa mwanahabari kutoka kwenye jimbo moja baada ya genge moja la watu kumpiga kwenye tukio la hadhara baada ya gavana wa jimbo kutokubaliana na ripoti zake.

Katika tamko lake kuhusu tukio la hivi karibuni la Fani-Kayode, Shirika la Amnesty International lilikemea tabia hii dhidi ya waandishi wa habari.

”Waandishi wa habari wanatafuta kuwajibisha viongozi kwa niaba ya watu na hawapaswi kutishiwa au kudhalilishwa kwa kuuliza maswali,” ilieleza taarifa ya shirika hilo.

Quote card. Mannir Dan Ali: "Afterwards, he insisted I take a wad of naira notes from him. I kept refusing and it took a long explanation for him to understand that I needed no incentive from him to do my job"

Ni wazi kabisa hili si jambo la mwisho kusikika kuhusu mahusiano mabaya kati ya vyombo vya habari na maafisa malimbali ambao ndio vyanzo vya habari.

Mbali na vitisho na mashambulizi ya maneno, pia kuna namna ambayo vyombo vya habari nchini Nigeria, na ninathubutu kusema pia katika nchi nyingine za kiafrika, vyombo vya habari hufanyiwa hila zinazosababisha wakashindwa kufanya kazi ipasavyo.

Baadhi ya mashirika ya serikali na makampuni makubwa hukataa kupeleka matangazo kwenye vyombo vya habari ambavyo havijawaripotia masuala yao kwa maslahi yao.

Halafu kuna ujira duni au hata kutolipwa kabisa mishahara na baadhi ya vyombo vya habari, ambayo inamaanisha kuwa waandishi wengine wana uaminifu kwa wale ambao wanaweza kulipa.

Wengine hutafuta pesa kabla ya kushughulikia kabla ya kushughulikia habari.

Kasri la ombaomba

Kwa uzoefu kama mwanahabari nchini Nigeria, sit u walio matajiri na wenye nguvu wanaofikiri kuwa waandishi wa habari ni watu wanaopokea tu.

Mfano mmoja wazi ulihusisha mkuu wa kikundi cha ombaomba katika jalala kubwa la taka huko Ijora Badia, makazi duni mjini Lagos.

Nilikuwa nimekwenda kumhoji nikiwa nafanya kazi na BBC mwishoni mwa miaka ya 1990 ili kujua kile alichofanya kuhusu jaribio la mamlaka kuwatoa ombaomba mitaani na kuingia katika kituo cha elimu ya kubadili tabia.

Alikuwa na mahakama aliyoiita kasri yake, iliyojengwa juu kabisa ya ncha kutoka kwa mbao zilizotupwa, ambapo alidhihaki pendekezo hilo.

Baadae alisisitiza anipatie fedha.

Someone counting 1,000 naira notes

Maelezo ya picha,

Baadhi ya waandishi huwa wanatarajia kulipwa baada ya kuripoti matukio

Niliendelea kukataa na ilinichukua muda mrefu kutoa maelezo kuwa sihitaji fedha yake ili kutekeleza wajibu wangu.

Hivi karibuni katika tukio la ubalozi wa Marekani kuadhimisha uhuru wa vyombo vya habari jijini Abuja, mwandishi mdogo wa habari alitaka kujua kwanini si sawa kuchukua fedha ili kuandika habari

Kwa maoni yake ni kuwa fedha zile ni sawa na zile zinazolipwa kwa wawakilishi kwenye semina na matukio mengine.

Msemaji mmoja katika hafla hiyo alielezea vizuri na methali, akisema “mkono wa mtoaji huwa chini ya mkono wa anayechukua” – akimaanisha kuwa wakati mwandishi wa habari anachukua fedha hizo, yeye hana uwezekano wa kutimiza wajibu wake ipasavyo au kuuliza maswali magumu.

Ni masikitiko Nigeria wakati huo nadra wakati maswali ya kutopendeza upande mmoja yanapoulizwa, mwandishi wa habari anaweza kupata majibu ya Fani-Kayode.

Presentational grey line

Source link

,Dakika 3 zilizopita Chanzo cha picha, One Voice Africa TV Maelezo ya picha, Waziri wa zamani wa Nigeria, Femi Fani-Kayode…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *