Jeshi la Uganda lawatafuta wafungwa takribani 200 waliotoroka katika gereza la Karamoja, on September 18, 2020 at 8:00 am

September 18, 2020

Jeshi nchini Uganda linaendelea na operesheni ya kuwatafuta zaidi ya wafungwa takribani 200 waliotoroka kutoka gereza kuu la Karamoja, kaskazini mashariki mwa Uganda siku ya Jumatano.Msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali Flavia Byekwaso amesema wafungwa hao waliojihami kwa silaha walizowapokonya askari wa magereza, wanaendelea na juhudi za kuwakamata wakiwa katika milima ya Moroto walikotorokea.Naibu Msemaji wa Jeshi la Uganda, linaloendesha oparesheni ya kuwasaka wafungwa waliotoroka kwenye gereza hilo la Moroto, Deo Akiiki, ameeleza walikofikia kwenye zoezi hilo la kuwasaka wafungwa hao alipozungumza na Mwandishi wa BBC Yusuph Mazimu.,

Jeshi nchini Uganda linaendelea na operesheni ya kuwatafuta zaidi ya wafungwa takribani 200 waliotoroka kutoka gereza kuu la Karamoja, kaskazini mashariki mwa Uganda siku ya Jumatano.

Msemaji wa jeshi Brigedia Jenerali Flavia Byekwaso amesema wafungwa hao waliojihami kwa silaha walizowapokonya askari wa magereza, wanaendelea na juhudi za kuwakamata wakiwa katika milima ya Moroto walikotorokea.

Naibu Msemaji wa Jeshi la Uganda, linaloendesha oparesheni ya kuwasaka wafungwa waliotoroka kwenye gereza hilo la Moroto, Deo Akiiki, ameeleza walikofikia kwenye zoezi hilo la kuwasaka wafungwa hao alipozungumza na Mwandishi wa BBC Yusuph Mazimu.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *