Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya lamshikilia kijana wa miaka 32 kwa tuhuma za mauaji, on September 15, 2020 at 10:00 am

September 15, 2020

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Bariki Kajuni mwenye miaka 32 ambaye ni mkazi wa  Makambako, Mkoa wa Njombe kwa tuhuma za kosa la mauaji ya Ansalemo Stawi Kisheria .Ansalemo Stawi Kisheria alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Zahanati ya Isangawana kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na mtuhumiwa.”Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliendelea na msako na mnamo tarehe 10.09.2020 majira ya saa 17:30 jioni huko Kitongoji na Kijiji cha Mgololo Mufindi, Wilaya ya Mafinga, Mkoa wa Iringa askari Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na askari wa Mafinga walimkamata mtuhumiwa”. Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.,

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Bariki Kajuni mwenye miaka 32 ambaye ni mkazi wa  Makambako, Mkoa wa Njombe kwa tuhuma za kosa la mauaji ya Ansalemo Stawi Kisheria .

Ansalemo Stawi Kisheria alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Zahanati ya Isangawana kwa matibabu baada ya kushambuliwa kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na mtuhumiwa.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya liliendelea na msako na mnamo tarehe 10.09.2020 majira ya saa 17:30 jioni huko Kitongoji na Kijiji cha Mgololo Mufindi, Wilaya ya Mafinga, Mkoa wa Iringa askari Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na askari wa Mafinga walimkamata mtuhumiwa”. 

Upelelezi unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *