Jeshi la polisi lawakamata watuhumiwa 48 wa makosa mbalimbali yakiwemo ya wizi, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 3), on September 4, 2020 at 10:00 am

September 4, 2020

 Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limefanya oparesheni na misako na kufanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 48 wa makosa mbalimbali’Msako huo umefanikisha  kupatikana kwa mafuta aina ya diesel lita 1,240, Mipira miwili ya kunyonyea mafuta ya wizi, mitambo ya kutengeneza pombe ya moshi (Gongo), Pombe ya moshi (Gongo) lita 124, viroba 10 vya mbegu za chia.Pia jeshi hilo limefanikiwa kukamata gari moja  aina ya Peugeot aliyokutwa nayo mtuhumiwa wa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu, simu za mkononi 85 za aina mbalimbali, Computer 6 zikiwa na Program za kuflash simu, na pikipiki 4, zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uporaji wa simu.”Tumeunda kikosi kazi cha kudhibiti matukio ya wizi wa simu za mkononi na kwa kipindi cha wiki mbili tumefanya oparesheni maalumu kwa kushirikiana na kitengo chá makosa ya wizi kwa njia ya mtandao na kufanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 41 wa matukio mbalimbali ya wizi wa simu, simu za mkononi 85 za aina mbalimbali, Computer 06 zikiwa na Program za kuflash simu, pikipiki 04 zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uporaji wa simu”.,

 Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limefanya oparesheni na misako na kufanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 48 wa makosa mbalimbali’

Msako huo umefanikisha  kupatikana kwa mafuta aina ya diesel lita 1,240, Mipira miwili ya kunyonyea mafuta ya wizi, mitambo ya kutengeneza pombe ya moshi (Gongo), Pombe ya moshi (Gongo) lita 124, viroba 10 vya mbegu za chia.

Pia jeshi hilo limefanikiwa kukamata gari moja  aina ya Peugeot aliyokutwa nayo mtuhumiwa wa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu, simu za mkononi 85 za aina mbalimbali, Computer 6 zikiwa na Program za kuflash simu, na pikipiki 4, zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uporaji wa simu.

“Tumeunda kikosi kazi cha kudhibiti matukio ya wizi wa simu za mkononi na kwa kipindi cha wiki mbili tumefanya oparesheni maalumu kwa kushirikiana na kitengo chá makosa ya wizi kwa njia ya mtandao na kufanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 41 wa matukio mbalimbali ya wizi wa simu, simu za mkononi 85 za aina mbalimbali, Computer 06 zikiwa na Program za kuflash simu, pikipiki 04 zilizokuwa zikitumika katika matukio ya uporaji wa simu”.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *