Jeshi la Lebanon limegundua tani 1.3 za fataki, on September 19, 2020 at 6:00 pm

September 19, 2020

 Jeshi la Lebanon limesema limefanikiwa kuzigundua tani 1.3 za fataki, baada ya msako uliofanyika katika bandari ya Beirut, ambayo mwezi uliopita iliharibika vibaya baada ya kutokea mripuko mkubwa, uliotokana na uhifadhi holela wa kiasi kikubwa cha kemikali. Katika taarifa ya jeshi iliyotolewa katika tovuti yake jana imesema kilo 1,320 za fataki zimepatikana kwenye mabokisi 120 yaliokuwa yamehifadhiwa katika ghala moja bandarini hapo. Bandari hiyo na sehemu kubwa ya katikati ya mji wa Beirut zilivurugwa vibaya na mripuko wa Agosti 4, ambao pia ulisababisha vifo vya watu 190. Ilielezwa chanzo cha mripuko huo ni shehena ya tani ya 2,750 kemikali ya ammonium nitrate ambayo ilihifadhiwa kwa namna duni.,

 

Jeshi la Lebanon limesema limefanikiwa kuzigundua tani 1.3 za fataki, baada ya msako uliofanyika katika bandari ya Beirut, ambayo mwezi uliopita iliharibika vibaya baada ya kutokea mripuko mkubwa, uliotokana na uhifadhi holela wa kiasi kikubwa cha kemikali. 

Katika taarifa ya jeshi iliyotolewa katika tovuti yake jana imesema kilo 1,320 za fataki zimepatikana kwenye mabokisi 120 yaliokuwa yamehifadhiwa katika ghala moja bandarini hapo. Bandari hiyo na sehemu kubwa ya katikati ya mji wa Beirut zilivurugwa vibaya na mripuko wa Agosti 4, ambao pia ulisababisha vifo vya watu 190. 

Ilielezwa chanzo cha mripuko huo ni shehena ya tani ya 2,750 kemikali ya ammonium nitrate ambayo ilihifadhiwa kwa namna duni.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *