Je sumu ya ricin iliotumwa kwa rais Trump kupitia barua ni ya aina gani?

September 21, 2020

Dakika 11 zilizopita

Maharage ya Castor yametumika kuzalisha sumu ya ricin , sumu hatari

Maelezo ya picha,

Maharage ya Castor yametumika kuzalisha sumu ya ricin , sumu hatari

Barua yenye sumu ya ricin ambayo ilikuwa imetumwa kwa rais wa Marekani Donald Trump imezuiwa kabla ya kufika White House.

Barua hiyo iligunduliwa katika katika ofisi ya ukaguzi wa vifurushi vya barua za maafisa wa gazi ya juu mjini Washingnton DC, maafisa walisema siku ya Jumamosi.

Ricin ni sumu hatari ambayo ishawahi kutumiwa katika shambulio la kigaidi siku zililizopita.

Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na maafisa wa ulinzi wa siri wanachunguza barua hiyo ilitumwa kutoka wapi na ikiwa kuna nyengine zilitumwa kupitia huduma za posta za Marekani.

“Kwa sasa hakuna tishio linalojulikana kwa usalama wa umma ,” FBI iliambia CNN katika taarifa siku ya Jumamosi.

Afisa wa ngazi ya juu serikalini ameambia The New York Times kwamba wachunguzi wanaamini kifurushi hicho kilitumwa kutoka Canada.

Uwepo wa ricin ulithibitishwa baada ya kupimwa na FBI.

FBI na majasusi wengine waligundua barua hiyo na kuizuia kabla ya kumfikia rais Trump

Polisi wa Canada waliripoti siku ya Jumamosi kuwa wanafanya kazi na mamlaka nchini Marekani kuchunguza “barua ya tuhuma.”

Ricin nini?

Ricin huzalishwa kutoka kwa usindikaji wa maharagwe ya castor, mmea katika familia ya Euphorbiaceae. Mbegu zake hutumiwa kutengeneza sumu.

Ni sumu hatari, ambayo kumeza, kuvuta harufu yake au kudungwa sindano, kunaweza kusababisha kichefu chefu, kutapika, kutokwa na damu ndani mwili na kuzuia viungo muhimu vya ndani kukosa kufanya kazi na hatimaye kifo.

Hakuna dawa ya kuikata makali

Mtu akishambuliwa na sumu hii anaweza kufariki baada ya kati ya saa 36 hadi 72, kulingana na kiwango cha dawa, kwa mjibu wa Kituo cha Marekani cha kudhibiti na Kuzuia magonjwa (CDC).

Risasi ya ricin ilitumika kumuua Georgi Markov , mchangiaji wa BBC 2018

Maelezo ya picha,

Risasi ya ricin ilitumika kumuua Georgi Markov , mchangiaji wa BBC 2018

Ricin ishawahi kutumiwa kufanya mashambulio ya kigaidi. Na inaweza kutengenezwa kuwa silaha kwa mfumo wa unga, gesi au chembe chembe.

Ikulu ya White House na majengo mengine ya umma yameshawahi kupokea kifurushi cha sumo ya ricin.

Mwaka 2014, mwanamume mmoja katika jimbo la Mississippi alifungwa miaka 25 jela kwa kumtumia barua iliyokuwa na sumu ya ricin kwa rais wa zamani Barack Obama na maafisa wake wengine.

Miaka minne baadae, 2018, afisa mkongwe wa jeshi la wanamaji alishutumiwa kwa kutuma barua iliyokuwa na sumu kwa Pentagon na White House.

Source link

,Dakika 11 zilizopita Chanzo cha picha, Getty Images Maelezo ya picha, Maharage ya Castor yametumika kuzalisha sumu ya ricin ,…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *