Je Simba Wanaweza Kukatwa Pointi KISA Kumtumia Benard Morrison?

October 3, 2020

Aliyewahi kuwa Mkurugenzi msaidizi wa kamati ya sheria na hadhi ya wanachama wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF Eliudi Peter Mvela amesema ili usajili wa mchezaji uwe umekamilika ni lazima kuwe na mkataba ambao unakidhi vigezo.

Mvela ametoa kauli hiyo alipokuwa kwenye mahojiano maalumu kwa njia ya simu na Kipenga ambapo amesema klabu ya Simba walipaswa kuwajibika kukamilisha mkataba wake na Benard Morrison maeneo yote ili kupata uhalali wa kumtumia kisha kusajiliwa ili kuidhinisha uhalali wa usajili wa mchezaji huyo.

“Nilichokiona mimi kama kina ukweli kuhusu mkataba uliooneshwa na Yanga ndio uliopelekwa na Simba kwenye shirikisho baasi Simba itakuwa wamefanya kosa kwakuwa kanuni zinakataa kuutambua mkataba ambao haujakamilika” amesema Mvela

Aidha, Mvela ameongeza kuwa TFF wana kanuni ambazo zinaeleza kuwa matatizo yoyote ya usajili yanapotokea kabla au baada ya pingamizi kupita inategemeana na hoja iliyokuwepo mbele yao.

Amesema hata kama mkataba utakua na mapungufu lakini mchezaji akawa amepewa kibali cha kufanya kazi ni wazi kuwa Timu husika haiwezi kupunguziwa alama alizozipata kwa kwenye michezo ila adhabu itakayotolewa ni ya udanganyifu.

“TFF lazima wamuwajibishe mtendaji wao aliyetenda kosa la kupitisha mkataba wenye mapungufu, pamoja na kufutiwa mkataba kwa mchezaji husika sambamba na kuidhibu klabu iliyotenda kosa hilo ila si kukatwa alama kwa kuwa kibali kilishatolewa” ameongeza Mvera

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *