Je ni kwanini vyakula vitokanavyo na mimea vimekuwa maarufu kwa Wamarekani weusi ?

September 13, 2020

Dakika 4 zilizopita

SUBMITTED PHOTO / MICHELLE LYN

Wamarekani weusi wana uwezekano mkubwa wa kula chakula kisichokuwa na nyama kuliko wazungu Wamarekani. Ni kwanini chakula hiki mbadala ni maarufu?

Wakati Louis Hunter alipoamka asubuhi tarehe 31 Mei hakujua ni nini cha kufanya.

Mji wa kwao wa Minneapolis ulikuwa umesambaratika baada ya wiki ya maandamano kufuatia kifo cha George Floyd, na biashara – ikiwemo mgahawa wake binafsi , Trio Plant-Based – ulikuwa umefungwa.

“Mungu alinigusa tu na akaniambia nenda nje na ugawe chakula chote ambacho nilikuwa nimekiandaa siku moja kabla, aliambia BBC.

Kwa ujumla, Bwana aligawa sahani 300 za chakula kisichokua na nyama pamoja na maji kwa waandamanaji wa vuguvugu la Black Lives Matter.

Mwaka 2016 alikuwa anakabiliwa na kifungo cha jela cha miaka 20 kutokana ma kushiriki maandamano ya ghasia baada ya kushiriki maandamano ya Black Lives Matter kufuatia kifo cha binamu yake , Philando Castile.

Bwana Hunter amekuwa akishikilia msimamo wake wa kuwa hakuwa na kosa, na mashitaka dhidi yake hatimaye yalipuuziliwa mbali, lakini akapoteza biashara yake kubwa na nyumba wakati alipokuwa katika kesi hiyo iliochukua zaidi ya mwaka mmoja.

Kupitia mapambano yake ya kisheria, alikutana na mwanaharakati mzungu Sarah Woodcock, ambaye alimfahamisha kwa mara ya kwanza dhana ya chakula kisicho na nyama al maarufu Vegasm.

Alianza kusoma kuhusu jinsi ya kupunguza na kuondoa vyakula vitokanavyo na wanyama vinavyoweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kusababisha magonjwa ya kudumu kama vile kisukari na shinikizo la damu – magonjwa ambayo yanaikumba zaidi jamii ya watu weusi nchini Marekani.

Wawili hao waliamua kuingia katika biashara , na baada ya msururu wa watu walioofika kununua bidhaa zao walifungua mgahawa uliojulikana kama Trio wakati wa majira ya vuli mwaka 2018. Na kwa sasa ni mmiliki wake, na kuufanya mgahawa wa Trio kuwa wa kwanza wa chakula kisicho na nyama unaomilikiwa na mtu mweusi katika jimbo lake.

Kwa mujibu wa utafiti wa Pew Research Center survey, 8% ya Wamarekani weusi hawali kabisa nyama, wakilinganishwa na 3% ya idadi ya watu wengine Wamarekani kwa ujumla.

Wakati huohuo, Wamarekani weusi maarufu kama vile Beyonce, Lizzo na mchezaji nyota wa tenisi Venus Williams sio walaji wa nyama au wanakula mara chache, huku Beyonce akishirikiana na ”migahawa ya vyakula vya mazao” kuwafikishia watu huduma ya vyakula hivyo nyumbani.

Muimbaji huyo aligonga vichwa vya habari miaka michache iliyopita alipoahidi kutoa tiketi za bure kwa matamasha yake ya mume wake Jay Z za maisha ambao watabadili milo yao na kula vyakula vitokanavyo na mimea pekee.

Lakini je ni kwanini vyakula vitonavyo na mimea vimekuwa maarufu kwa Wamarekani weusi ?

‘Kuifunza jamii yangu’

Kwa watu weusi wanaokula vyakula vya mimea, safari yao huanza kwa nia ya kuishi maisha ya kiafya.

Wamarekani weusi wana viwango vikubwa vya magonjwa ya shinikizo la damu, kisukari aina ya pili, unene wa mwili wa kupindukia na saratani kuliko makundi mengine ya watu. Kwa sehemu moja ikisababishwa na aina ya vyakula na vinywaji wanavyokula vyenye chumvi nyingi, mafuta na kiwango kidogo cha matunda na mboga, utafiti unaonesha.

Je vyakula vitokanavyo na mimea ni vya afya?

Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa kuna uwezekano wa kupungua kwa hatari ya mtu kuwa na magonjwa ya kudumu anapokula vyakula hivi.

Kiwango cha chakula, kando na thamani ya chakula, pia ni kigezo muhimu cha kuimarisha uzito wa mwili unaofaa kiafya.

Masuala haya yameyatia msukumo mashirika kadhaa yanayomilikiwa na watu weusi, kama vile Compton Vegan, kutoa vyakula vitokanavyo na mimea kwa miji ya ndani inayokaliwa na jamii za weusi.

Mamia waliandamana kushinikiza umuhimu wa kula chakula cha afya 2017 katia ene jirani la Washington DC

Maelezo ya picha,

Mamia waliandamana kushinikiza umuhimu wa kula chakula cha afya 2017 katia ene jirani la Washington DC

Lakini vyakula hivyo sio lazima viwe na utando wa mafuta mengi, Hunter ,anasema , Menyu katika mgahawa wa Trio imekonga mioyo ya wateja wanaopenda vyakula vizuri, akitumia vitu kama viungo vinavyopatia muonekano mzuri mboga.

Kwa mara ya kwanza , wengi wa wateja wake walikuwa wazungu, lakini kwa sasa karibu nusu ya wateja wake ni weusi.

‘Kujiona binafsi ukiwakilishwa ‘

Kwa Omowale Adewale, ambaye ni mwakilishi wa tamasha la vyakula vitokanavyo na mimea Black VegFest, lililoanzishwa na watu weusi kwa ajili ya jami ya watu weusi mjini New York City, kuunganisha ulaji wa vyakula vya mimea na utamaduni wa watu weusi ni muhimu.

Omowale Adewale mwanzilishi wa Black Vegfast

Lakini kuanzishwa kwa tamasha hilo kwa mara ya kwanza, kuliangaliwa kama kitu cha ajabu na wazungu wengi wanaokula vyakula hivyo vitokanavyo na mimea.

” Jamii inayokula vyakula vitokanavyo na mimea imekuwa ni ya wazungu kwa muda mrefu, na wakati mwingine inaonekana kama wanataka kuufanya utamaduni huu wa kula vyakula vya mimea kuwa ni wa wazungu tu,” anasema.

Huku mashirika mengi yanayopigia debe ulaji wa vyakula vitokanavyo na mimea kwa ajili ya kuboresha hali za wanyama, pia Black VegFest haitofautiani nayo, Bwana Adewale pia huhakikisha ukumbi wake unazungumzia masuala katika jamii za weusi kama vile mapambano dhidi ya kumaliza ukatili wa polisi.

Vyakula asilia vya Kiafrika, huku vikiwa sio vitokanavyo na mimea tu, kwa kiasi kikubwa hutokana na vyakula vya mimea na vina majani ya kijani kibichi mboga za aina tofauti – vyakula asilia kwa afya .

Katika utafiti wa hivi karibu uliowahusisha watu 48,000 wenye umri wa zaidi ya miaka 18 ulilinganisha afya ya walaji wa nyama, na wengine wanaokula samaki na kunywa maziwa lakini wasiokula nyama – na wanaokula vyakula vitokanavyo na mimea.

Walibaini kuwa watu wanaokula vyakula vitokanavyo na mimea wana hatari ya kiwango cha chini cha kupata ugonjwa wa moyo, lakini wana hatari ya kiwango cha juu ya kupata kiharusi, huenda kutokana na ukosefu wa vitamin B12.

‘Vuguvugu la walaji wa vyakula vya mimea pia lina mizizi ya muda mrefu ya uhusiano na Vuguvugu la Haki za kiraia. Dick Gregory, mwanaharakati maarufu na mchekeshaji aliyekuwa karibu na Martin Luther King, aliacha kula nyama mwaka 1965 .

‘Kula vizuri kupigana vita’

Alikuwa ni Gregory ambaye alianzisha Tracye McQuirter kwa ajili ya walaji wa vyakula vitokanavyo na mimea kwa zaidi ya miaka 30 iliyopita , wakati alipotoa hotuba kwa wanafunzi weusi katika taasisi ya mafunzo ya Amherst College

Sasa, Bi McQuirter ni mmoja wa waandishi wengi na washawishi ambao wanasaidia kuhamasisha ulaji wa vyakula vya mimea miongoni mwa jamii ya watu weusi .

Kitabu chake cha mapishi cha 2010 kilichoandikwa na Any Greens , kiliandikwa kwa ajili ya wanawake weusi, na mwaka huu anazindua kampeni ya mtandaoni kujaribu kuwapata wanawake 10,000 weusi wa kuanza kula vyakula vitokanavyo na mimea.

Tracye McQuirter

Maelezo ya picha,

Tracye McQuirter anawataka watu weusi kula vizuri ili kupigana vita vilivyopo mbele yao

Bi McQuirter anasema kwamba ulaji wa vyakula vitokanavyo na mimea ni muhimu zaidi sasa kuliko awali, kwani Covid-19 ikiikumba jamii ya watu weusi, kwa sehemu moja kwasababu ya viwango vyao vya juu vya magonjwa ya kudumu waliyonayo hata kabla ya kupata maambukizi

Huku maelfu wakiandamana katika maandamano ya Black Lives Matter Bi McQuirter anasema ni “dharura kwetu kujitunza wenyewe na kula vyema ili tuwe na nguvu za kupigana vita hivi “.

Source link

,Dakika 4 zilizopita Chanzo cha picha, SUBMITTED PHOTO / MICHELLE LYN Wamarekani weusi wana uwezekano mkubwa wa kula chakula kisichokuwa…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *