Jaribio la Chanjo ya Chuo kikuu cha Oxford lasimamishwa baada ya mshiriki kuugua, on September 9, 2020 at 6:00 am

September 9, 2020

Majaribio ya mwisho ya kimatibabu kwa ajili ya chanjo ya virusi vya corona , iliyotengenezwa na AstraZeneca pamoja na Chuo Kikuu cha Oxford yamesitishwa baada ya mshiriki kuugua kutokana na athari za majaribio hayo.AstraZeneca imeelezea kusitishwa huko kwa jaribio hilo “kwa kawaida” pale inapotokea “kuugua kusiko eleweka”.Matokeo ya majaribio ya chanjo yanafuatiliwa kwa karibu kote duniani.Chanjo ya AstraZeneca-na Cho Kikuu cha Oxford inaonekana kama yenye ushindani mkubwa wa makumi kadhaa ya chanjo zinazotengenezwa katika maeneo mengine ya duniani.Matumaini yalikua ya hali ya juu kwamba chanjo hiyo ingeweza kuwa moja ya chanjo za kwanza kuingia katika soko la chanjo, kufuatia mafanikio yake ya awali ya kipimo cha awamu ya kwanza na cha awamu ya pili.Jaribio lake la kwenda katika awamu ya tatu katika wiki za hivi karibuni limewahusisha washiriki wapatao 30,000 nchini Marekani pamoja na Uingereza, Brazil na Afrika Kusini. Majaribio ya awamu ya tatu ya chanjo kwa kawaida huwahusisha maelfu ya washiriki na yanaweza kudumu kwa miaka kadhaa.,

Majaribio ya mwisho ya kimatibabu kwa ajili ya chanjo ya virusi vya corona , iliyotengenezwa na AstraZeneca pamoja na Chuo Kikuu cha Oxford yamesitishwa baada ya mshiriki kuugua kutokana na athari za majaribio hayo.

AstraZeneca imeelezea kusitishwa huko kwa jaribio hilo “kwa kawaida” pale inapotokea “kuugua kusiko eleweka”.

Matokeo ya majaribio ya chanjo yanafuatiliwa kwa karibu kote duniani.

Chanjo ya AstraZeneca-na Cho Kikuu cha Oxford inaonekana kama yenye ushindani mkubwa wa makumi kadhaa ya chanjo zinazotengenezwa katika maeneo mengine ya duniani.

Matumaini yalikua ya hali ya juu kwamba chanjo hiyo ingeweza kuwa moja ya chanjo za kwanza kuingia katika soko la chanjo, kufuatia mafanikio yake ya awali ya kipimo cha awamu ya kwanza na cha awamu ya pili.

Jaribio lake la kwenda katika awamu ya tatu katika wiki za hivi karibuni limewahusisha washiriki wapatao 30,000 nchini Marekani pamoja na Uingereza, Brazil na Afrika Kusini. Majaribio ya awamu ya tatu ya chanjo kwa kawaida huwahusisha maelfu ya washiriki na yanaweza kudumu kwa miaka kadhaa.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *