Jaji mwandamizi katika mahakama ya juu zaidi ya Hong Kong ajiuzulu, on September 18, 2020 at 1:00 pm

September 18, 2020

Mmoja wa majaji 14 wa kigeni katika mahakama ya juu zaidi ya Hong Kong amejiuzulu kwa sababu ya wasiwasi juu ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyowekwa na China. Ofisi ya kiongozi wa jimbo la Hong Kong Carrie Lam imethibitisha kujiuzulu kwa jaji raia wa Australia James Spigelman lakini haikutoa sababu ya kujiuzulu kwake.Spigelman, ambaye ni jaji mkuu wa zamani wa New South Wales, amekuwa jaji mwandamizi wa kwanza kujiuzulu na kuikosoa hadharani sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyopitishwa na bunge la China.Jaji huyo ameliambia shirika la habari la Australia la ABC, kuwa alijiuzulu kutokana na sababu zinazohusiana na yaliyomo kwenye sheria ya usalama wa kitaifa japo hakutoa ufafanuzi zaidi.Kujiuzulu kwake kunajiri wakati ambapo kuna ukosoaji mkubwa wa sheria hiyo mpya ya usalama katika jimbo la Hong Kong ambalo liliwahi kutawalia na Uingereza.,

Mmoja wa majaji 14 wa kigeni katika mahakama ya juu zaidi ya Hong Kong amejiuzulu kwa sababu ya wasiwasi juu ya sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyowekwa na China. 

Ofisi ya kiongozi wa jimbo la Hong Kong Carrie Lam imethibitisha kujiuzulu kwa jaji raia wa Australia James Spigelman lakini haikutoa sababu ya kujiuzulu kwake.Spigelman, ambaye ni jaji mkuu wa zamani wa New South Wales, amekuwa jaji mwandamizi wa kwanza kujiuzulu na kuikosoa hadharani sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyopitishwa na bunge la China.

Jaji huyo ameliambia shirika la habari la Australia la ABC, kuwa alijiuzulu kutokana na sababu zinazohusiana na yaliyomo kwenye sheria ya usalama wa kitaifa japo hakutoa ufafanuzi zaidi.

Kujiuzulu kwake kunajiri wakati ambapo kuna ukosoaji mkubwa wa sheria hiyo mpya ya usalama katika jimbo la Hong Kong ambalo liliwahi kutawalia na Uingereza.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *