Jaji Ginsburg wa mahakama kuu Marekani afariki

September 19, 2020

Jaji Ruth Bader Ginsburg wa mahakama kuu ya Marekani amefariki duniani Ijumaa mjini Washington. Alikuwa na umri wa miaka 87.

Ginsburg alikuwa mwanamke wa pili kuteuliwa kushika nafasi katika mahakama hiyo na hadi kufa kwake alikuwa mmoja wa majaji watatu wanawake katika mahakama hiyo ya juu kabisa nchini Marekani. Wengine ni Sonia Sotomayor and Elena Kegan.

Ginsburg alikuwa pia mmoja wa majaji wenye msimamo wa kiliberali katika mahakama hiyo yenye jumla ya majaji tisa.

Afya ya Ginsburg ilikuwa dhoofu katika miaka ya hivi karibuni, akiingia na kutoka hoispitali mara kadha. Ripoti za awali zinasema amefariki kutokana na saratani.

Source link

,Jaji Ruth Bader Ginsburg wa mahakama kuu ya Marekani amefariki duniani Ijumaa mjini Washington. Alikuwa na umri wa miaka 87….

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *