Jafo aahidi kutoa kipaumbele kwa waliosoma nje, on September 19, 2020 at 3:00 pm

September 19, 2020

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, amesema kuwa atahakikisha watanzania waliosoma nje wanapewa kipaumbele katika suala la kupata ajira serikalini.Jafo amesema hayo leo, Septemba, 19,2020,  wakati anahutubia katika Mahafali ya Kimataifa ya wahitimu waliosoma nje yaliyofanyika Mlimani City Jijini, Dar es salaam, ameahidi kuwapigia debe vijana hao na kuhakikisha katika nafasi walizotoa wanashughulikiwa.”Nikuhakikishieni tutajitahidi kwa kadri tutakavyotangaza nafasi za ajira, wasomi waliosoma nje kwa ada za wazazi waliohangaika lazima watapata kipaumbele” amesema Waziri Jafo.Aidha Jafo ameusifu utaratibu wa kuwapeleka vijana kwenda kusoma nje kuwa ni utaratibu  utaokasaidia nchi kupanda kiuchumi, “Kwa utaratibu huu kama tukijipanga vizuri kwa pamoja serikali na sekta binafsi kwa pamoja yale malengo ya nchi yetu kuzidi kupaa kiuchumi yatafikiwa”.,

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, amesema kuwa atahakikisha watanzania waliosoma nje wanapewa kipaumbele katika suala la kupata ajira serikalini.

Jafo amesema hayo leo, Septemba, 19,2020,  wakati anahutubia katika Mahafali ya Kimataifa ya wahitimu waliosoma nje yaliyofanyika Mlimani City Jijini, Dar es salaam, ameahidi kuwapigia debe vijana hao na kuhakikisha katika nafasi walizotoa wanashughulikiwa.

“Nikuhakikishieni tutajitahidi kwa kadri tutakavyotangaza nafasi za ajira, wasomi waliosoma nje kwa ada za wazazi waliohangaika lazima watapata kipaumbele” amesema Waziri Jafo.

Aidha Jafo ameusifu utaratibu wa kuwapeleka vijana kwenda kusoma nje kuwa ni utaratibu  utaokasaidia nchi kupanda kiuchumi, “Kwa utaratibu huu kama tukijipanga vizuri kwa pamoja serikali na sekta binafsi kwa pamoja yale malengo ya nchi yetu kuzidi kupaa kiuchumi yatafikiwa”.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *