Jacob Blake atuma ujumbe kwa wafuasi wake kutoka hospitalini

September 7, 2020

Dakika 5 zilizopita

Jacob Blake atuma ujumbe kwa wafuasi wake kutoka hospitalini

Jacob Blake, mwanaume mweusi ambaye alipigwa risasi mara saba na polisi mzungu katika jimbo la Wisconsin nchini Marekani mwezi uliopita, amesema ana maumivu yaisiyoisha katika video aliyotuma kwenye mtandao.

Bwana Blake, ambaye familia yake inasema anaweza kupooza kuanzia sehemu ya kiuno, pia alitoa ujumbe wa matumaini, akisema kuna “mengi ya kunifanya niishi “.

Blake mwenye umri wa miaka 29 alipigwa risasi mgongoni wakati alipokuwa akikamatwa.

Tukio la kupigwa kwake risasi liliibua tena wimbi la maandamano juu ya ubaguzi wa rangi na ukatili nchini Marekani.

Baadhi ya maandamano katika mji wa Kenosha, ambako Bwana Blake alipigiwa risasi, yaligeuka na kuwa ghasia, huku watu wawili wakiuawa.

Uchunguzi juu ya kupigwa risasi kwa Bwana Blake unaendelea.

Wakati huo huo, Bwana Blake alifikishwa mahakamani Ijumaa, akakana mashitaka ya uhalifu dhidi yake yaliokuwa yamewasilishwa kabla ya kupigwa risasi

Ni nini alichosema Bwana Blake?

Katika video iliyotumwa kwenye mtandao wa Twitter na wakiili wa familia yake, Bwana Blake-bado anaonekana akiwa kwenye kitanda cha hospitali-akizungumzia juu ya maumivu anayoyapata.

“Kila saa 24 ni maumivu, hakuna lolote ila maumivu. Inaumiza kupumua, inaumiza kulala, inaumiza kugeuka upande mmoja kuelekea mwingine, inaumiza kula ,” alisema.

Dadake jacob Blake

“Maisha yako, na sio maisha yako tu, miguu yako, kitu unachokihitaji utembee na kuendeleza maisha, vinaweza kuchukuliwa kama hivi ,” alisema, huku akigongesha vidole vyake.

“Muwe na umoja , tengenezeni pesa, fanya mambo kuwa rahisi kwa watu wetu, kwasababu kuna muda mwingi ambao umepotezwa ,” aliongeza

Je ufyatuaji risasi ulitokeaje?

Afisa wa polisi alimpiga risasi Bwana Blake wakati alipokuwa akijaribu kumkamata alipokuwa akijaribu kuingia ndani ya gari ambamo kulikuwa na watoto wake watatu wameketi.

Bwana Blake hakuwa na silaha wakati alipopigwa risasi lakini baadae kisu kilipatikana ndani ya gari lake lilipofanyiwa uchunguzi na wapelelezi.

Video za ufyatuaji wa risasi ambazo ziliwekwa kwenye mtandao, zilichochea msururu wa maandamano katika mji wa Kenosha, ambayo yaligeuka kuwa ghasia katika baadhi ya maeneo . Waandamanaji wawili waliuawa wakati wa uporaji na uharibifu wa mali . Kijana mwenye umri wa miaka 17 ameshitakiwa kwa mauaji.

Rais Donald Trump na mgombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden walitembelea mji huo.

Bwana Biden alizungumza kwa njia ya simu na Bwana Blake na kukutana na ndugu zake. Alitoa wito kwa afisa aliyempiga risasi Blake mgongoni akamatwe.

Rais Trump hakukutana na familia ya Bwana Blake, akisema ni kwasababu alitaka mawakili wawepo.

Source link

,Dakika 5 zilizopita Chanzo cha picha, Twitter Jacob Blake, mwanaume mweusi ambaye alipigwa risasi mara saba na polisi mzungu katika…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *