Italia bado ipo katika mtikisiko wa kifo cha Kijana Mweusi, on September 12, 2020 at 5:00 pm

September 12, 2020

Mamia ya watu nchini Italia wamejitokeza leo hii katika mazishi ya kijana mweusi, ambae aliuwawa kwa kipigo cha kikatili, ambacho kimelitingisha taifa hilo na kusababisha lawama kutoka katika ngazi za juu za serikali.Waziri Mkuu Giuseppe Conte na waziri wa mambo ya ndani wa Italia walihudhuria mazishi ya Willy Monteiro Duarte, kijana wa umri wa miaka 21, mwenye asili ya Cape Verde ambae aliuwawa Septemba 6, katika ugomvi uliozuka mjini Colleferro,ambao upo katika viunga vya Roma.Watu wanne raia wa Italia wamekamatwa na polisi, wakiwemo ndugu wawili, ingawa hadi sasa waendesha mashitaka hawajaonesha kama mauwaji hayo yanatokana na msukumo wa ubaguzi wa rangi.,

Mamia ya watu nchini Italia wamejitokeza leo hii katika mazishi ya kijana mweusi, ambae aliuwawa kwa kipigo cha kikatili, ambacho kimelitingisha taifa hilo na kusababisha lawama kutoka katika ngazi za juu za serikali.

Waziri Mkuu Giuseppe Conte na waziri wa mambo ya ndani wa Italia walihudhuria mazishi ya Willy Monteiro Duarte, kijana wa umri wa miaka 21, mwenye asili ya Cape Verde ambae aliuwawa Septemba 6, katika ugomvi uliozuka mjini Colleferro,ambao upo katika viunga vya Roma.

Watu wanne raia wa Italia wamekamatwa na polisi, wakiwemo ndugu wawili, ingawa hadi sasa waendesha mashitaka hawajaonesha kama mauwaji hayo yanatokana na msukumo wa ubaguzi wa rangi.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *