Israel na Lebanon kufanya mazungumzo ya mpaka wa baharini,

October 2, 2020

 

Lebanon na Israel zimesema jana kuwa zitafanya mazungumzo yatakayosimamiwa na Marekani juu ya mpaka wao wa baharini wanaouzozania. Marekani imeitaja hatua hiyo kuwa ni ya kihistoria kati ya nchi hizo mbili. Lebanon inataka kuchimba gesi ya asilia ya hidrokaboni katika eneo la bahari ya Mediterania linalozozaniwa na Israel. Mjumbe maalumu wa Marekani David Schenker amesema mazungumzo hayo yamepangwa kufanyika Oktoba 14. Lebanon na Israeli wamekuwa wakigombania mpaka huo kwa miongo kadhaa. Nchi hizo mbili hazina uhusiano rasmi wa kidiplomasia na zinaendelea kuwa katika hali ya vita. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mazungumzo hayo yatafanyika katika ofisi za Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *