Iran yazionya UAE, na Bahrain kuhusu makubaliano na Israel, on September 17, 2020 at 1:00 pm

September 17, 2020

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kwamba Umoja wa falme za kiarabu na Bahrain zitawajibika na athari za aina yoyote zitakazosababishwa na hatua yao ya kuingia kwenye mikataba ya kurudisha uhusiano wa kawaida na Israel ambayo ni hasimu mkubwa wa Iran.Tamko la rais huyo wa Iran limekuja siku moja baada ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mawaziri wa mambo ya nje wa Bahrain na Umoja wa Falme za kiarabu kusaini makubaliano ya kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia katika sherehe iliyofanyika katika ikulu ya Marekani. Rouhani akizungumza katika mkutano wa baraza la mawaziri nchini Iran amesema Israel inatekeleza vitendo vingi vya uhalifu katika ardhi ya Wapalestina kila siku na kuhoji inawezekana vipi kuuinyooshea mkono Israel. Rais Donald Trump wa Marekani amesema makubaliano mengine kama hayo yanakaribia kufanyika kati ya Israel na nchi ngine nyingi za kiarabu ikiwemo hasimu mkubwa wa Iran katika ukanda huo,Saudi Arabia.,

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema kwamba Umoja wa falme za kiarabu na Bahrain zitawajibika na athari za aina yoyote zitakazosababishwa na hatua yao ya kuingia kwenye mikataba ya kurudisha uhusiano wa kawaida na Israel ambayo ni hasimu mkubwa wa Iran.

Tamko la rais huyo wa Iran limekuja siku moja baada ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na mawaziri wa mambo ya nje wa Bahrain na Umoja wa Falme za kiarabu kusaini makubaliano ya kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia katika sherehe iliyofanyika katika ikulu ya Marekani. 

Rouhani akizungumza katika mkutano wa baraza la mawaziri nchini Iran amesema Israel inatekeleza vitendo vingi vya uhalifu katika ardhi ya Wapalestina kila siku na kuhoji inawezekana vipi kuuinyooshea mkono Israel. 

Rais Donald Trump wa Marekani amesema makubaliano mengine kama hayo yanakaribia kufanyika kati ya Israel na nchi ngine nyingi za kiarabu ikiwemo hasimu mkubwa wa Iran katika ukanda huo,Saudi Arabia.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *