Iran yatekeleza hukumu ya kifo dhidi ya mpiganaji miereka

September 13, 2020

Iran imesema imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya mpiganaji miereka mmoja Navid Afkari hapo jana kwa kumuuwa mwanamume mmoja wakati wa maandamno dhidi ya serikali katika mwaka wa 2018 na kuibua shutuma kali na mshtuko kwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa – IOC.Mwendesha mashtaka mkuu wa mkoa Kazem Mosuavi, alinukuliwa katika wavuti wa televisheni ya kitaifa akisema kuwa Afkari wa umri wa miaka 27 aliuliwa katika gereza moja katika mji wa Shiraz Kusini mwa nchi hiyo.Idara ya mahakama ilisema kuwa Afkari alipatikana na hatia ya ”mauaji ya hiari” kwa kumdunga kisu Hossein Torkman, mnamo Agosti 2 mwaka 2018.Kamati ya IOC imesema kuwa imeshtushwa na mauaji hayo na kwamba ”inakera mno” kwamba miito ya wanariadha kote duniani na mashirika ya kimataifa ilishindwa kuzuia hatua hiyo.Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alilaani hatua hiyo na kusema wanaishtumu vilivyo.Aliongeza kuwa ni shambulizi kali dhidi ya utu wa binadamu na kwamba sauti za raia wa Iran hazitanyamazishwa.,

Iran imesema imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya mpiganaji miereka mmoja Navid Afkari hapo jana kwa kumuuwa mwanamume mmoja wakati wa maandamno dhidi ya serikali katika mwaka wa 2018 na kuibua shutuma kali na mshtuko kwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa – IOC.
Mwendesha mashtaka mkuu wa mkoa Kazem Mosuavi, alinukuliwa katika wavuti wa televisheni ya kitaifa akisema kuwa Afkari wa umri wa miaka 27 aliuliwa katika gereza moja katika mji wa Shiraz Kusini mwa nchi hiyo.

Idara ya mahakama ilisema kuwa Afkari alipatikana na hatia ya ”mauaji ya hiari” kwa kumdunga kisu Hossein Torkman, mnamo Agosti 2 mwaka 2018.

Kamati ya IOC imesema kuwa imeshtushwa na mauaji hayo na kwamba ”inakera mno” kwamba miito ya wanariadha kote duniani na mashirika ya kimataifa ilishindwa kuzuia hatua hiyo.

Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alilaani hatua hiyo na kusema wanaishtumu vilivyo.

Aliongeza kuwa ni shambulizi kali dhidi ya utu wa binadamu na kwamba sauti za raia wa Iran hazitanyamazishwa.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *