Ijue kauli mbiu ya CHADEMA, Lissu aifafanua, noreply@blogger.com (Muungwana Blog), on August 29, 2020 at 6:00 pm

August 29, 2020

Mgombe wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameweka wazi kuwa kauli mbiu itakoyobeba ilani yao ya chama ni Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania.Amesema hayo hii leo Agosti 29, 2020, wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho kwa Jimbo la Kawe, ambapo amesema, chochote kilichopo kwenye ilani kinabeba msingi wa kauli mbiu hizo..”Ilani yetu ya Uchaguzi Mkuu huu ina kauli mbiu yenye maneno yafuatayo, Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu, chochote ambacho tumekisema katika ilani hii msingi wake ni uhuru wa watu msingi wa watu na maendeleo ya watu”, amesema Lissu.Aidha Tundu Lisuu amesema kuwa maendeleo wanayaoyataka yatazingatia uhuru, haki na maendeleo ya Watanzania kama yale aliyoyaita Baba wa Taifa maendeleo ya watu.”Maendeleo tunayoyataka ni yanayozingatia uhuru wa watu, yanayozingatia haki zao, maendeleo aliyoyaita Baba wa Taifa maendeleo ya watu badala ya vitu”, ameongeza.,

Mgombe wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameweka wazi kuwa kauli mbiu itakoyobeba ilani yao ya chama ni Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania.

Amesema hayo hii leo Agosti 29, 2020, wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho kwa Jimbo la Kawe, ambapo amesema, chochote kilichopo kwenye ilani kinabeba msingi wa kauli mbiu hizo..

“Ilani yetu ya Uchaguzi Mkuu huu ina kauli mbiu yenye maneno yafuatayo, Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu, chochote ambacho tumekisema katika ilani hii msingi wake ni uhuru wa watu msingi wa watu na maendeleo ya watu”, amesema Lissu.

Aidha Tundu Lisuu amesema kuwa maendeleo wanayaoyataka yatazingatia uhuru, haki na maendeleo ya Watanzania kama yale aliyoyaita Baba wa Taifa maendeleo ya watu.

“Maendeleo tunayoyataka ni yanayozingatia uhuru wa watu, yanayozingatia haki zao, maendeleo aliyoyaita Baba wa Taifa maendeleo ya watu badala ya vitu”, ameongeza.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *