Ijue historia ya mchezaji wa soka Serge Aurier, noreply@blogger.com (Muungwana Blog 2), on August 28, 2020 at 7:30 pm

August 29, 2020

Desemba 24, 1992 alizaliwa mchezaji wa soka wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu a Tottenham Serge Aurier. Alizaliwa katika mji wa Kusini Kati wa Ouragahio nchini Ivory Coast.Hucheza katika safu ya ulinzi ya pembeni kulia. Alianza katika klabu mbalimbali za vijana klabu ya kutua Villepent nchini Ufaransa.Akiwa huko Villepent alionekana na klabu ya Lens iliyoko Ligi Kuu nchini humo Ligue 1 ambako aliingia katika soka la kulipwa.Akiwa na umri wa miaka 13 alijiunga na Lens. Juni 2009 alisaini rasmi mkataba na Lens. Aurier alienda Ufaransa akiwa mtoto na alikulia huko akifanikiwa kuzitumikia klabu za Lens, Toulouse na Paris Saint Germain akishinda jumla ya mataji 11.Amecheza mechi 169 katika Ligue 1 na akitajwa mara mbili katika Timu Bora ya Mwaka ya Ligi hiyo. Mnamo mwaka 2017 alijiunga na Spurs kwa ada ya pauni milioni 23. Katika timu ya taifa aliitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 mpaka sasa akiwa ameshacheza mechi 50.Aliiwakilisha Ivory Coast katika Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil na mara tatu katika michuano ya mataifa ya Ulaya  na alitwaa taji la Afrika mwaka 2015 akiwa na Tembo hao wa Afrika.,

Desemba 24, 1992 alizaliwa mchezaji wa soka wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu a Tottenham Serge Aurier. Alizaliwa katika mji wa Kusini Kati wa Ouragahio nchini Ivory Coast.

Hucheza katika safu ya ulinzi ya pembeni kulia. Alianza katika klabu mbalimbali za vijana klabu ya kutua Villepent nchini Ufaransa.

Akiwa huko Villepent alionekana na klabu ya Lens iliyoko Ligi Kuu nchini humo Ligue 1 ambako aliingia katika soka la kulipwa.

Akiwa na umri wa miaka 13 alijiunga na Lens. Juni 2009 alisaini rasmi mkataba na Lens. Aurier alienda Ufaransa akiwa mtoto na alikulia huko akifanikiwa kuzitumikia klabu za Lens, Toulouse na Paris Saint Germain akishinda jumla ya mataji 11.

Amecheza mechi 169 katika Ligue 1 na akitajwa mara mbili katika Timu Bora ya Mwaka ya Ligi hiyo. Mnamo mwaka 2017 alijiunga na Spurs kwa ada ya pauni milioni 23. Katika timu ya taifa aliitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2013 mpaka sasa akiwa ameshacheza mechi 50.

Aliiwakilisha Ivory Coast katika Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil na mara tatu katika michuano ya mataifa ya Ulaya  na alitwaa taji la Afrika mwaka 2015 akiwa na Tembo hao wa Afrika.,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *