Ijue historia ya mchezaji wa mpira David Villa,

October 5, 2020

 

Desemba 3, 1981 alizaliwa mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Barcelona David Villa.

Kwa sasa nyota huyo anaitumikia klabu ya Japan ya Vissel Kobe. Villa amekuwa akichukuliwa kuwa miongoni mwa washambuliaji bora katika kizazi chake pia amekuwa akichukuliwa kuwa miongoni mwa washambuliaji bora wa Hispania wa zama zote.

Amekuwa akifahamika kwa jina la utani El Guaje kwa maana ya mtoto na jina hilo alilipata kutokana na kwamba wakati akianza kucheza mpira alikuwa akicheza na watoto wenzake ambao wamemzidi umri.

Akiwa mtoto aliwahi kupata majeruhi lakini baadaye alianza maisha ya soka akiwa na klabu ya Sporting Gijon mnamo mwaka 2001. Baada ya hapo alikwenda Real Zaragoza kwa misimu miwili ambako alicheza mechi za La Liga pia kutwaa Kombe la Mfalme, na Supercopa de España.

Alijiunga na Valencia mwaka 2005 kwa ada ya euro milioni 12 ambako alitwaa tena Kombe la Mfalme. Akiwa na umri wa miaka 28 alikuwa tayari ameshafika mabao 28 katika Ligi Kuu.

Ndipo Barcelona walipomwona mwaka 2010. Walimchukua kwa ada ya euro milioni 40 ambako alitwaa La liga kwa mara ya kwanza na mataji ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. Mnamo mwaka 2011 katika fainali ya Ligi ya Mabingwa alifunga.

Aliondoka Barcelona mnamo mwaka 2013 na kwenda zake Atletico Madrid kwa ada ya euro milioni 5.1 ambako alitwaa taji la Ligi Kuu.

Baada ya msimu mmoja huko Madrid aliondoka na kwenda zake nchini Marekani katika klabu ya New York City  na akiwa huko aliweka rekodi ya kuwa mfungaji wa zama zote wa klabu hiyo.

Mnamo mwaka 2016 alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Marekani. Mwaka 2018 Villa alitangaza kuondoka New York City na kutua zake nchini Japan katika klabu aliyopo sasa ya Vissel Kobe.
,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *