IGP Sirro kuongoza tena shirikisho la wakuu wa polisi mashariki mwa Afrika (EAPCCO), on September 18, 2020 at 10:00 am

September 18, 2020

Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika (EAPCCO) wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kuendelea kuwa mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja.Uamuzi huo umetolewa leo na nchi 14 wanachama wa Shirikisho hilo kupitia mkutano wake mkuu wa 22 wa mwaka uliofanyika kwa njia ya mtandao (video conference) ambapo Wakuu hao waliona kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Corona kumesababisha mambo mengi ya shirikisho hilo kutokamilika kwa wakati.Hata hivyo IGP Sirro alisema kuwa, hadi sasa Shirikisho hilo limepata mafanikio makubwa huku akieleza kuwa katika kipindi cha 2021 wamejipanga kutekeleza yale ambayo hayakuweza kufikiwa na watahakikisha kuwa nchi wanachama wataweza kubadilishana uzoefu na kufanya mafunzo ya pamoja ya mbinu za medani. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma IGP Sirro alisema kuwa, kutokana na ushirikiano wa Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika kumewezesha kudhibiti uhalifu wa kupanga na unaovuka mipaka, usafirishaji wa nyara za serikali sambamba na kudhibiti biashara haramu ya usafirishaji binadamu na dawa za kulevya, alisema IGP Sirro.Aidha, IGP Sirro anaendelea tena kuongoza shirikisho hilo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja tangu pale alipochaguliwa katika mkutano mkuu wa 21 wa mwaka uliofanyika mwezi Septemba mwaka jana jijini Arusha. ,

Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika (EAPCCO) wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kuendelea kuwa mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja.

Uamuzi huo umetolewa leo na nchi 14 wanachama wa Shirikisho hilo kupitia mkutano wake mkuu wa 22 wa mwaka uliofanyika kwa njia ya mtandao (video conference) ambapo Wakuu hao waliona kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Corona kumesababisha mambo mengi ya shirikisho hilo kutokamilika kwa wakati.

Hata hivyo IGP Sirro alisema kuwa, hadi sasa Shirikisho hilo limepata mafanikio makubwa huku akieleza kuwa katika kipindi cha 2021 wamejipanga kutekeleza yale ambayo hayakuweza kufikiwa na watahakikisha kuwa nchi wanachama wataweza kubadilishana uzoefu na kufanya mafunzo ya pamoja ya mbinu za medani. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma IGP Sirro alisema kuwa, kutokana na ushirikiano wa Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika kumewezesha kudhibiti uhalifu wa kupanga na unaovuka mipaka, usafirishaji wa nyara za serikali sambamba na kudhibiti biashara haramu ya usafirishaji binadamu na dawa za kulevya, alisema IGP Sirro.

Aidha, IGP Sirro anaendelea tena kuongoza shirikisho hilo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja tangu pale alipochaguliwa katika mkutano mkuu wa 21 wa mwaka uliofanyika mwezi Septemba mwaka jana jijini Arusha. 

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *