IGP Sirro amemtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha Polisi,

October 1, 2020

 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amemtaka mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Tundu lissu kuripoti kituo cha Polisi Moshi Kilimanjaro kutokana na kitendo chake alichokifanya jana akiwa mkoani humo.

IGP Sirro amesema hayo leo ambapo alimtaka Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Freeman Mbowe kukaa na watu wake wazungumze suala la utii wa sheria bila shuruti.

Aidha IGP Sirro ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limepewa mamlaka ya kulinda usalama wa raia na mali zao huku akiwaeleza kuwa hakuna mtu yeyote anayeweza kupambana na Jeshi hilo na kwamba wote wanaovunja sheria za nchi watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *