Hussein Mwinyi kuwapa Wazanzibar fursa za ajira na soko la kuuza bidhaa zao, on September 14, 2020 at 1:00 pm

September 14, 2020

 NA Thabit madai, ZANZIBAR.MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba iwapo atateuliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha anakuza utalii wa Zanzibar ambao utawanufaisha Wazanzibar kwa kupata  fursa za ajira na soko  la kuuza bidhaa zao.Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa ziara maalumu ya kuwatembelea wananchi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kusini Unguja, ikiwa ni muendelezo wake wa kampenni za urais kupitia chama hicho cha mapinduzi CCM.Dk Mwinyi amesema moja ya kipaumbele chake endapo atachaguliwa na wananchi uwa Rais wa Zanzibar kukuza utalii na kufikia utalii wa hali ya juu   ambapo utalii huo utakwenda kuwanufaisha Wazanzibar kwa kupata ajira kwa wingi pamoja na kuuza bidhaa zao mbalimbali ambazo watazizalisha.Amesema anafahamu katika utalii ambao upo kwa sasa unakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo wawekezaji ndani katika sekta hiyo kuwanyanyasa fanyakazi wa mahoteli pamoja na kuwanyima baadhi ya haki zao za msingi na kuahidi atalishughulikia endapo atachaguliwa rais wa Zanzibar.Katika Maelezo yake Dk Mwinyi amesema kwamba atahakikisha kuwa anatatua changamoto zote ambazo zinawakabili wavuvi na uvuvi visiwani Zanzibar na kuanzisha viwanda ambavyo vitachakata samaki na kuuza.Amesema kuwa atahakikisha anaanzisha viwanda vya uchakati wa samaki ndani ya visiwani hivyo na kuwanufaiisha wananchi kwa kupata ajira za kubwa na ndogo ndogo.“Lazima tuhakikishe kwamba uvuvi na wavuvi wanatuliwa changamoto zinazowakabilia sambamba n kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki ambavyo vitawanufaisha wananchi visiwani humo”amesema DK Mwinyi.Nao Wananchi wamesema kwamba changamoto kubwa inayowakabili katika sekta ya utalii ni unyanyasaji na ukoseshwaji wa haki kutoka kwa waajiri wao.“Nimesikia kuwa kuna changamoto kubwa katika sekta ya utalii ikiwemo hao wawekezaji na waajiri ndani ya sekta hiyo kuwanyanyasa na wafnyakazi ambao ni wazawa, hivyo ntahakikisha natatua kero hiyo na kukuza utaliii ambao utawanufaisha kila mmoja kwa kupata ajira za uhakika”amesema Dk Mwinyi.Wamesema vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji wao wakiwa kazini huwa vimekithiri kwa kiasi kikubwa na kuwakosesha haki zao za msingi ikiwemo kufukuzwa kihorera na kumuomba mgombea huyo kuwasimamia endapo atachaguliwa kuwa Rais wa ZanzibarNae Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Zanzibar Abdallah Juma Sadala alimaarufu Mabodi amesema kwamba CCM Imedhamiria kufanya kampeni za kistaarabu ambao watawafuata wananchi katika maeneo ya husika na kuwasliza changamoto zinazowakabili na kuwaahidi kuwatatulia.Dk Mwinyi amesema wataendelea na utaratibu huo wa kufanya kampeni kwa kuwafuata wananchi kuwasilikiza ili wanapoingia madarakani uwatatulia bila ya upendeleo.Katika Ziara hiyo Dk Mwinyi ametembela eneo la kizimkazi Dimbani, Kizimkazi Mkunguni Makunduchi na Jambiani kibigija katika Mkoa wa Kusini Unguja.,

 NA Thabit madai, ZANZIBAR.

MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba iwapo atateuliwa kuwa Rais wa Zanzibar atahakikisha anakuza utalii wa Zanzibar ambao utawanufaisha Wazanzibar kwa kupata  fursa za ajira na soko  la kuuza bidhaa zao.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa ziara maalumu ya kuwatembelea wananchi katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa kusini Unguja, ikiwa ni muendelezo wake wa kampenni za urais kupitia chama hicho cha mapinduzi CCM.

Dk Mwinyi amesema moja ya kipaumbele chake endapo atachaguliwa na wananchi uwa Rais wa Zanzibar kukuza utalii na kufikia utalii wa hali ya juu   ambapo utalii huo utakwenda kuwanufaisha Wazanzibar kwa kupata ajira kwa wingi pamoja na kuuza bidhaa zao mbalimbali ambazo watazizalisha.

Amesema anafahamu katika utalii ambao upo kwa sasa unakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo wawekezaji ndani katika sekta hiyo kuwanyanyasa fanyakazi wa mahoteli pamoja na kuwanyima baadhi ya haki zao za msingi na kuahidi atalishughulikia endapo atachaguliwa rais wa Zanzibar.

Katika Maelezo yake Dk Mwinyi amesema kwamba atahakikisha kuwa anatatua changamoto zote ambazo zinawakabili wavuvi na uvuvi visiwani Zanzibar na kuanzisha viwanda ambavyo vitachakata samaki na kuuza.

Amesema kuwa atahakikisha anaanzisha viwanda vya uchakati wa samaki ndani ya visiwani hivyo na kuwanufaiisha wananchi kwa kupata ajira za kubwa na ndogo ndogo.

“Lazima tuhakikishe kwamba uvuvi na wavuvi wanatuliwa changamoto zinazowakabilia sambamba n kuanzisha viwanda vya kuchakata samaki ambavyo vitawanufaisha wananchi visiwani humo”amesema DK Mwinyi.

Nao Wananchi wamesema kwamba changamoto kubwa inayowakabili katika sekta ya utalii ni unyanyasaji na ukoseshwaji wa haki kutoka kwa waajiri wao.

“Nimesikia kuwa kuna changamoto kubwa katika sekta ya utalii ikiwemo hao wawekezaji na waajiri ndani ya sekta hiyo kuwanyanyasa na wafnyakazi ambao ni wazawa, hivyo ntahakikisha natatua kero hiyo na kukuza utaliii ambao utawanufaisha kila mmoja kwa kupata ajira za uhakika”amesema Dk Mwinyi.

Wamesema vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji wao wakiwa kazini huwa vimekithiri kwa kiasi kikubwa na kuwakosesha haki zao za msingi ikiwemo kufukuzwa kihorera na kumuomba mgombea huyo kuwasimamia endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Zanzibar Abdallah Juma Sadala alimaarufu Mabodi amesema kwamba CCM Imedhamiria kufanya kampeni za kistaarabu ambao watawafuata wananchi katika maeneo ya husika na kuwasliza changamoto zinazowakabili na kuwaahidi kuwatatulia.

Dk Mwinyi amesema wataendelea na utaratibu huo wa kufanya kampeni kwa kuwafuata wananchi kuwasilikiza ili wanapoingia madarakani uwatatulia bila ya upendeleo.

Katika Ziara hiyo Dk Mwinyi ametembela eneo la kizimkazi Dimbani, Kizimkazi Mkunguni Makunduchi na Jambiani kibigija katika Mkoa wa Kusini Unguja.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *