Human Right Watch lasema Rwanda ilikiuka sheria za kimataifa katika kumkamata Rusesababiga

September 11, 2020

Dakika 1 iliyopita

Paul Rusesabagina

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema kukamatwa kwa mkosoaji wa chama tawala cha Rwanda RPF Paul Rusesababagina ni sawa na kulazimishwa kutoweka, ambao ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa.

Shirika hilo limesema Rwanda inapaswa kumpatia Bwana Rusesababigina fursa ya kuwasiliana na mawakili ambao amewachagua yeye, mawasiliano ya siri na kumuwezesha kuwasiliana na familia yake mara kwa mara.

Bwana Rusesabagina alikamatwa mjini Dubai katika Muungano wa nchi za kiarabu tarehe 27 Agosti na tarehe 31 mwezi huo ofisi ya upelelezi nchini Rwanda RIB ikatangaza kuwa yupo katika mahabusu zake baada ya kumuonesha waandishi wa habari.

Rusesabagina ambaye alipata umaarufu kutokana na filamu ya mauaji ya kimbari Hotel Mille Collines, alikuwa kiongozi wa makundi ya watu wenye silaha, FNL miongoni mwao, na ambalo hivi karibuni lilianzisha mshambulizi dhidi ya Rwanda na kuua watu Kusini Magharibi.

Rusesabagina pia alikuwa naibu kiongozi wa vuguvugu la upinza la MRCD lililodai kuhusika na mashambulio dhidi ya maeneo ya kusini magharibi mwa Rwanda mwaka 2018.

Shirka la Human Rights Watch linasema Rwanda inapaswa kumpa mtuhumiwa huyo haki ya kisheria ya kupinga kisheria kukamatwa kwake na kuwakilishwa na mawakili aliowachagua yeye mbele ya mahakama huru inayofuata sheria za kimataifa za haki za binadamu.

“Rwanda imejenga rekodi ya kutumia njia zisizo za kisheria kuwalenga wale inaowaona kama tisho kwa chama tawala ,” alisema Lewis Mudge, mkurugenzi wa Human Rights Watch, kanda ya Afrika ya kati katika taarifa ya shirika hilo kwa waandishi wa habari.

Rusesabagina alizungumza na familia yake kwa njia ya simu tarehe 8 Septemba. Hata hivyo mmoja wa watu wa familia yake anadaiwa kuliambia shirika hilo kuwa walikuwa na wasiwasi kwasababu hakuwa anazungumza kwa uhuru kwasababu mawakili wake wawili hawakuwepo wakati wa mazungumzo hay.

Rais Kagame alisema nini juu ya Rusesabagina

Rais wa Rwanda Paul Kagame alisema Rusesababigina hakutekwa nyara, alidanganwa akajileta mwenye Rwanda.

Alisema kikubwa siyo ushujaa wa Bwana Rusesabagina au vitendo vyake wakati wa mauaji ya kimbari akisema kinachoangaliwa kwa sasa ni yeye kuwajibishwa kuhusu vitendo alivyotaja kuwa vya mauaji dhidi ya raia wa Rwanda katika matangazo ya moja kwa moja kwa televisheni ya taifa Jumapili jioni,

Bwana Kagame alisema kwamba hajali kuhusu hadithi ya Bwana Rusesabagina kwamba yeye ni shujaa wa mauaji ya kimbari na kwamba ”hilo si jambo litakalomkabili mahakamani”.

“Kuna maswali ambayo lazima atayajibu…kuna wanaomsaidia wakiwa Ulaya, Marekani na kwingineko na ambao walimpandisha cheo na kumpa majina ya ushujaa. Awe shujaa au la ,mimi sina wasi wasi na hilo.

”Kikubwa tunachoangalia hapa ni kuhusika kwake na mauaji dhidi ya raia wa Rwanda, damu ya wananchi wa Rwanda iliyoko mikononi mwake kutokana na yeye kuongoza makundi ya kigaidi, lazima atawajibishwa kwa hayo” Alisema Rais Kagame.

Aliongeza kuwa Paul Rusesabagina alikuwa kiongozi wa makundi ya watu wenye silaha, FNL miongoni mwao, na ambapo hivi karibuni lilianzisha mshambulizi dhidi ya Rwanda na ”kuua watu Kusini Magharibi”

”Rusesabagina ametoa maelezo kabla hajafika hapa, mwenyewe akisifia jambo hilo.” Rais Kagame alisema.

Paul Rusesabagina, ni kiongozi wa muungano wa kisasa MRCD-Ubumwe ambacho Rwanda inauuhusisha na mashambulio ya ugaidi yaliyowaua Wanyarwanda katika kituo cha polisi cha mjini Kigali.

Rusesabagina ambaye alikuwa anaishi ukimbizini Marekani na Ubelgiji, kwa tukio la kushtukiza alioneshwa kwa vyombo vya habari Jumatatu iliyopita katika ofisi za shirika la upelelezi la Rwanda.

Ofisi ya upelelezi ya Rwanda (RIB) ilisema nini?

Ofisi ya Rwanda ya upelelezi (RIB) ilisema kwa urefu kwamba jina la Bwana Rusesabagina lilikua miongoni mwa majina yaliyopo kwenye waranti ya kimataifa, kwa ajili ya kukamatwa na kuwasilishwa katika mahakama za Rwanda.

Ofisi ya Rwanda ya upelelezi (RIB) ilisema kuwa Bwana Rusesabagina alikamatwa kwa ushirikiano wa kimataifa.

”Rusesabagina anakabiliwa na mashitaka kadhaa ikiwa ni pamoja na ugaidi, utekaji, kuchoma moto mali na mauaji”, alisema kaimu msemaji wa Ofisi ya Rwanda ya upelelezi (RIB) Dkt Thierry Murangira .

Bwana Murangira aliwaambia waandishi wa habari kuwa uhalifu anaodaiwa kuufanya aliutekeleza dhidi ya Wanyarwanda ambao hawakuwa na silaha, wasio na hatia kwenye ardhi ya Rwanda ikiwa ni pamoja na mashambulizi yaliyotekelezwa katika wilaya ya Nyaruguru Juni 2018, Nyungwe, na Wilaya ya Nyamagabe Disemba 2018.

Familia yake ilisema nini?

Akizungumza na BBC baada ya baba yake kufika Rwanda, mtoto wa kike wa Bwana Rusesabagina -Anaïse Kanimba alisema :”alitekwa nyara alipokuwa safarini Dubai “, katika Muungano wa nchi za kiarabu (UAE).”

“Alifika Jumanne, ndio mara ya mwisho tulipozungumza nae akituambia kuwa amefika salama, hatukumsikia tena hadi tulipoona kuwa amekamatwa na utawala wa Rwanda”.

“Hatujui alifikaje huko na kilichotokea, ndio maana tunafikiria kuwa alitekwa kwasababu asingeenda Rwanda kwa hiari yake.”

Anaishi uhamishoni Marekani na ni raia wa Ubelgiji , aliongeza.

“Kwahiyo tungependa nchi hizi mbili zitusaidie kumrudisha nyumbani.

“Mashitaka wanayomshitaki hayana msingi ,” Bi Kanimba aliongeza katika mahojiano na kipindi cha BBC Newsday.

Ni nini kinachoendelea kuhusu kesi ya Rusesabagina

Kesi ya Paul Rusesababigina bado haijaanza kusikilizwa.

Kwa sasa anazuiliwa na vyombo vya usalama kwa mashitaka ya ugaidi, kutekeleza mali kwa moto na kuua.

Alhamisi ilifanyika kesi dhidi ya washirika wa zamani wa Rusesabagina -Callixte Nsabimana maarufu Sankara na Herman Nsengimana aliyechukua nafasi ya msemaji wa kundi la FLN baada ya Sankara kukamatwa

Mahakama ilijadili maombi ya mwendesha mashitaka ya kuoanisha kesi ya waliokuwa wasemaji wa kundi hilo kwa nyakati tofauti,Callixte Nsabimana maarufu Sankara na Herman Nsengimana aliyechukua naasi ya usemani wa kundi la FLN baada ya Sankara kukamatwa.

Source link

,Dakika 1 iliyopita Chanzo cha picha, BBC GAHUZA Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Rights Watch limesema…

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *