“Huku nikitaka kuku-cheat inanijia sura yako ukilia mbele ya waandishi” Roma,

October 5, 2020

Msanii wa HipHop Roma Mkatoliki ametimiza miaka mitano ya ndoa yake na mkewe Mrs. Roma, ambapo wamesheherekea kwa kutumiana ujumbe wa kupongezana na kutakiana kheri kwa walipo na wanapoelekea.

Kupitia ukurasa wa Instagram Roma Mkatoliki ameandika “Nakumbuka kipindi kile miaka zaidi ya 11 iliyopita, ulivyokuwa unanitongoza nakukatalia, ukanitongoza mara ya pili nikakuchomolea ukawa unalia sanaa daaaah, mara ya tatu nikaja kukuonea huruma nikakukubalia tukaanza mahusiano, leo tuna miaka mitano kwenye ndoa yetu hakika Yehova ni mwaminifu“

“Huku kila nikitaka kuku-cheat inanijia ile sura yako ukilia mbele ya waandishi wa habari kipindi nimetekwa, ikinijia tu basi hisia zote zinakata naishiwa nguvu nawafukuzia mbali wazungu, navuta shuka nalala peke yangu, Mungu aendelee kudumisha ndoa yetu usiache kuniombea Shetani asije akanihadaa nami nafanya hivyo pia“Roma

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *