Hiki ndicho kitu kiinachoongeza thamani yako sana, on September 6, 2020 at 7:30 pm

September 6, 2020

Kwa kawaida ipo hivi, ili uweze kutengeneza mafanikio ni lazima uweze kutoa thamani kwa uhakika. Kila mtu atakapoangalia kazi yako au kile unachokifanya ni lazima aone ubora na utofauti mkubwa juu ya kitu hicho ukifanyacho.Inawezekana ukawa unajua thamani ni hali ya kuwa katika ubora, hadi kuwafanya wengine wakutamani wewe au watamani huduma yako unayoitoa.  Kitu cha kujiuliza je, unajua thamani ya kitu chochote inatengenezwa na nini?Hapa kwenye swali hilo juu ndipo wengi wanaanza kushindwa, wanakuwa ni watu kweli ambao wanataka thamani kubwa katika maisha yao, lakini kwa bahati mbaya hawajui hiyo thamani ambayo itawapa mafanikio inapatikana vipi na wapi.Thamani yoyote unayoitafuta kwenye maisha yako uelewe, imejificha kwenye muda. Upo ulazima wa wewe kutumia muda wa kutosha ili kutengeneza thamani yako. Kama unakimbilia kutengeneza thamani ndani ya muda mfupi, huo ni uongo.Waangalie watu ambao wana thamani kubwa sana na kwa maana hiyo pia watu hao wana mafanikio makubwa. Watu hao ukiwaangalia walitumia muda mwingi sana katika kutengeneza thamani hiyo ambayo imewapa mafanikio hayo mafanikio makubwa.Ukiona mtu thamani yake inaonekana ni kubwa lakini imepatikana kwa muda mfupi, nikwambie tu thamani hiyo ni ya muda mfupi na wakati utafika thamani hiyo itatoka na yale mafanikio yataporomoka na ushindwe kuamini ni kitu gani kilitokea.Kwa hiyo kama unaona maisha yako yameshuka au maisha yako hayasogei kama vile utakavyo wewe, amua kupandisha thamani yako. Kwa bahati mbaya sana thamani yako hiyo haiji kwa bahati mbaya bali ni kwa wewe kujituma na kujipa muda.Kweli ukidhamiria kuongeza thamani yako na kuwa mtu wa tofauti hilo linawezekana. Anza leo kubadilisha thamani yako kwa kusoma vitabu sana vya mafanikio na hilo litaleta mabadiliko makubwa sana ya maisha yako na kwa kiasi kikubwa.Ukumbuke thamani uliyonayo inabadili maisha yako sana.  Hakuna ambaye anashindwa kwenye maisha au atashindwa kupata pesa kama mtu huyo hana thamani kubwa ndani yake. Mafanikio ni lazima kama ndani yako una thamani ya kutosha.Usikubaki kuishi kizembe, kila wakati jaribu kujiuliza ni kitu gani nifanye ili niongeze thamani yangu na kuwa bora na bora. Kwa kukijua kitu hicho na kukifanya, basi unakuwa upo kwenye wakati sahihi wa kufanikiwa kwako.Kitu kinachoongeza thamani yako zaidi ni matumizi ya muda. Weka hili akilini na fanyia kazi kila wakati. Kwa kufanya hivyo hapo utafanikiwa na kutengeneza mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa ujumla.Kama unataka mafanikio ya muda mrefu na wewe hakikisha unatengeneza au ndani mwako una thamani ya muda mrefu sana. Thamani hiyo kama nilivyosema haipatikani hivi hivi tu, ipo kwenye muda, ni lazima kujipa muda wa kutengeneza thamani hiyo.Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.,

Kwa kawaida ipo hivi, ili uweze kutengeneza mafanikio ni lazima uweze kutoa thamani kwa uhakika. Kila mtu atakapoangalia kazi yako au kile unachokifanya ni lazima aone ubora na utofauti mkubwa juu ya kitu hicho ukifanyacho.

Inawezekana ukawa unajua thamani ni hali ya kuwa katika ubora, hadi kuwafanya wengine wakutamani wewe au watamani huduma yako unayoitoa.  Kitu cha kujiuliza je, unajua thamani ya kitu chochote inatengenezwa na nini?

Hapa kwenye swali hilo juu ndipo wengi wanaanza kushindwa, wanakuwa ni watu kweli ambao wanataka thamani kubwa katika maisha yao, lakini kwa bahati mbaya hawajui hiyo thamani ambayo itawapa mafanikio inapatikana vipi na wapi.

Thamani yoyote unayoitafuta kwenye maisha yako uelewe, imejificha kwenye muda. Upo ulazima wa wewe kutumia muda wa kutosha ili kutengeneza thamani yako. Kama unakimbilia kutengeneza thamani ndani ya muda mfupi, huo ni uongo.

Waangalie watu ambao wana thamani kubwa sana na kwa maana hiyo pia watu hao wana mafanikio makubwa. Watu hao ukiwaangalia walitumia muda mwingi sana katika kutengeneza thamani hiyo ambayo imewapa mafanikio hayo mafanikio makubwa.

Ukiona mtu thamani yake inaonekana ni kubwa lakini imepatikana kwa muda mfupi, nikwambie tu thamani hiyo ni ya muda mfupi na wakati utafika thamani hiyo itatoka na yale mafanikio yataporomoka na ushindwe kuamini ni kitu gani kilitokea.

Kwa hiyo kama unaona maisha yako yameshuka au maisha yako hayasogei kama vile utakavyo wewe, amua kupandisha thamani yako. Kwa bahati mbaya sana thamani yako hiyo haiji kwa bahati mbaya bali ni kwa wewe kujituma na kujipa muda.

Kweli ukidhamiria kuongeza thamani yako na kuwa mtu wa tofauti hilo linawezekana. Anza leo kubadilisha thamani yako kwa kusoma vitabu sana vya mafanikio na hilo litaleta mabadiliko makubwa sana ya maisha yako na kwa kiasi kikubwa.

Ukumbuke thamani uliyonayo inabadili maisha yako sana.  Hakuna ambaye anashindwa kwenye maisha au atashindwa kupata pesa kama mtu huyo hana thamani kubwa ndani yake. Mafanikio ni lazima kama ndani yako una thamani ya kutosha.

Usikubaki kuishi kizembe, kila wakati jaribu kujiuliza ni kitu gani nifanye ili niongeze thamani yangu na kuwa bora na bora. Kwa kukijua kitu hicho na kukifanya, basi unakuwa upo kwenye wakati sahihi wa kufanikiwa kwako.

Kitu kinachoongeza thamani yako zaidi ni matumizi ya muda. Weka hili akilini na fanyia kazi kila wakati. Kwa kufanya hivyo hapo utafanikiwa na kutengeneza mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa ujumla.

Kama unataka mafanikio ya muda mrefu na wewe hakikisha unatengeneza au ndani mwako una thamani ya muda mrefu sana. Thamani hiyo kama nilivyosema haipatikani hivi hivi tu, ipo kwenye muda, ni lazima kujipa muda wa kutengeneza thamani hiyo.

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatimia.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *