Heche: Mkinichagua matatizo ya maji bai bai, on September 14, 2020 at 1:00 pm

September 14, 2020

 Na Timothy Itemba Mara.Mgombea ubunge jimbo la Tarime vijijini,John Heche ameomba wapiga kura kuendelea kuwa na imani wakati walipomchagua kuwaongoza sasa anawaomba kumuongezea kipindi kingine cha miaka 5 ili kuingia bungeni na kumaliza tatizo la kero ya maji  kuwa historia.Akiongeza katika viwanja vya mji wa Nyamongo alisema kuwa akifanikiwa na kuwa mbunge atahakikisha Tarime vijijini wanaondokana na tatizo la kero ya maji lililopo kwa sasa na kuwa watatumia fedha inayolipwa na mgodi.Heche aliongeza kuwa kama wananchi wakiendelea kumwamini na kumchagua kwa kumpa kura zitakazomwezesha kutangazwa na kuwa mbunge atahakikisha mji wa Nyamongo unakuwa na mamalaka ya mji mdogo kamili ili kusogeza huduma karibu na wananchi. “Nimefanya maendeleo awamu iliyopita nimesimamia fedha zinazotoka mgodini na kuhaklikisha wananchi mnapata maendeleo sasa nawaombeni tena kunipa kura za kutosha zitakazoniwezesha kutangazwa ili kuwa mbunge.Nikitangazwa na kuwa mbunge Nyamongo itakuwa na mamlaka mji mdogo ili huduma za wananchi kuwa karibu pia nikiwa mbunge kero na tatizo la maji Nyamongo itakuwa Bay bay”alisema Heche.Naye diwani mstaafu,Agostine Marwa Sasi aliwaondoa wasiwasi wapiga kura kuwa wakichagua upinzani hawatakuwa na maendeleo ambapo alisema kuwa maendeleo hayana chama.Sasi aliongeza kusema kuwa wananchi wasifanye kosa badala yake wamchague  Heche ili aende bungeni akawatumikie na swala la maendeleo atasimamia kwasababu halmashauri ya Tarime vijijini inapokea fedha nyingi kutoka mgodi zainazotekeleza miradi nikodi ya wananchi wanazolipa kwasbabu hiyo maendeleo hayana budi kuja.,

 

Na Timothy Itemba Mara.

Mgombea ubunge jimbo la Tarime vijijini,John Heche ameomba wapiga kura kuendelea kuwa na imani wakati walipomchagua kuwaongoza sasa anawaomba kumuongezea kipindi kingine cha miaka 5 ili kuingia bungeni na kumaliza tatizo la kero ya maji  kuwa historia.

Akiongeza katika viwanja vya mji wa Nyamongo alisema kuwa akifanikiwa na kuwa mbunge atahakikisha Tarime vijijini wanaondokana na tatizo la kero ya maji lililopo kwa sasa na kuwa watatumia fedha inayolipwa na mgodi.

Heche aliongeza kuwa kama wananchi wakiendelea kumwamini na kumchagua kwa kumpa kura zitakazomwezesha kutangazwa na kuwa mbunge atahakikisha mji wa Nyamongo unakuwa na mamalaka ya mji mdogo kamili ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

 “Nimefanya maendeleo awamu iliyopita nimesimamia fedha zinazotoka mgodini na kuhaklikisha wananchi mnapata maendeleo sasa nawaombeni tena kunipa kura za kutosha zitakazoniwezesha kutangazwa ili kuwa mbunge.

Nikitangazwa na kuwa mbunge Nyamongo itakuwa na mamlaka mji mdogo ili huduma za wananchi kuwa karibu pia nikiwa mbunge kero na tatizo la maji Nyamongo itakuwa Bay bay”alisema Heche.

Naye diwani mstaafu,Agostine Marwa Sasi aliwaondoa wasiwasi wapiga kura kuwa wakichagua upinzani hawatakuwa na maendeleo ambapo alisema kuwa maendeleo hayana chama.

Sasi aliongeza kusema kuwa wananchi wasifanye kosa badala yake wamchague  Heche ili aende bungeni akawatumikie na swala la maendeleo atasimamia kwasababu halmashauri ya Tarime vijijini inapokea fedha nyingi kutoka mgodi zainazotekeleza miradi nikodi ya wananchi wanazolipa kwasbabu hiyo maendeleo hayana budi kuja.

,

Article Categories:
Habari

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *